Makonda apewa siku saba kesi ya Guninita

Makonda apewa siku saba kesi ya Guninita

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
Makonda-17April2015.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda

17th April 2015

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imetoa siku saba kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda, kuwasilisha utetezi wake dhidi ya kesi ya madai iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida, Mgana Msindai na Mwenyekiti CCM mkoa Dar es Salaam, John Guninita.

Kesi hiyo namba 68 ya 2015, Makonda alitakiwa kuwasilisha utetezi wake mahakamani jana, lakini wakili kupitia wakili wake, Lusiu Peter, ameomba Mahakama kumuongezea muda.

Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa amekubali ombi la utetezi na ametoa siku saba kwa Makonda kuwasilisha uetetezi wake hadi Aprili 23, mwaka huu.

Hakimu Riwa alisema kesi hiyo itatajwa Aprili 27,mwaka huu.

Katika kesi ya msingi, Msindai na Guninita wanaiomba mahakama hiyo kumuamuru Makonda awaombe msamaha na kumlipa kila mmoja Sh. milioni 100.

Wanadai fidia hiyo kutokana na maneno ya kuwadhalilisha yanayodaiwa kutolewa na Makonda kama Katibu Uhamasishaji na Chipukizi wa CCM katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Msindai na Guninita kupitia wakili wao, Benjamini Mwakagamba, wanaiomba Mahakama pamoja na mambo mengine itoe zuio la kudumu kwa Makonda asizungumze tena maneno ya kashfa wala kuyasambaza kama alivyofanya awali.

CHANZO: NIPASHE
 
Wana Ukumbi,

Waswahili wanasema kimya kingi kina mshindo mkubwa!

Ikiwa na baada ya vijana wa CCM kuamua kumpeleka Dr Slaa mahakamani kwa kauli zake za udhalilishaji, hilo pia limefanywa kwa Paul Makonda.

Makonda amekokotwa mahakamani na viongozi wa CCM kufuatia kauli yake ya kumdhalilisha Lowassa ambayo aliitoa sambamba na kudhalilisha vigogo wengine wa chama ikiwa ni pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Dar es salaam, ndugu John Buninita na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai.

Maamuzi haya ya kwenda mahakamani yamechelewa kufanywa ikiwa ni kutokana na kushindwa kwa shinikizo la kumtaka Makonda aombe radhi kupitia njia ile ile aliyotumia kutoa kashfa zake dhidi ya vigogo hao.

Vigogo hao wametoa madai ya kila mmoja kutaka Kiasi cha milioni 100 pesa za Kitanzania ikitokea Makonda ameshindwa kuthibitisha ukweli wa kashfa zake katika utetezi wake afikapo Mahakamani, ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempa siku saba kutoa utetezi wake huo.
 
Taarifa yako haijakamilika. Je Makonda amepelekwa mahakama ipi na mashtaka yake ni yepi. Ni lini Makonda kapelekwa maHAKAMANI?
 
Safi Sana then makonda usiwe Kama zitto bdo kijana Mdgo anza mwanzo vizur Kama wenzio akina January makamba,John mnyika la sivyo utapotea Kama kumbikumbi ndani ya siasa
 
mahakani ndio mdudu gani?
kwanini una post mada nyingi nyingi, huoni unatukera kwa kutujazia saver na kutusumbua huku mada yenyewe haina kichwa wala miguu???

cc
mleta mada
 
Ujinga kama huu hauwezi kushinda ukweli ufisadi wa lowasa hawezi kisafishwa na mahakama kamwe atabaki fisadi tu.

Acha ujinga wewe, nchi hii hairuhusu kutukana watu. Acha kuficha maovu kwa mahaba ya mtu fulani. Kama ana ushahidi wa aliyokuwa anayasema sasa ndo yupo sehemu muafaka wa kuutoa
 
Yaani na ww ni kilaza. Warioba kasema hajapigwa. Ww unasema warioba kapigwa. Mmh! Vp mm nikisema ww umelawitiwa.
Ni wapi Warioba alisema hajapigwa? nakumbuka mara ya mwisho Warioba alisema wazi kapigwa na Makonda..... Mzee Butiku alimkemea Makonda hadharani..... Mzee Mkapa juzi alikemea utaratibu wa uteuzi wa viongozi wa umma akilenga uteuzi wa Makonda, mtu anayepiga wazee na kutukana viongozi.....
 
Hawa wazee niliwah kuleta habar yao hapa kjpitia mwananchi newspaper wakimtaka Makonda aombe radhi,ni muda mrefu umepita nikajua yameisha kumbe walimaanisha.
Nakumbuka waliasema kuwa rais hajashauriwa vzuri kumteua Makonda.Ntaisaka ile Link
 
Ni wapi Warioba alisema hajapigwa? nakumbuka mara ya mwisho Warioba alisema wazi kapigwa na Makonda..... Mzee Butiku alimkemea Makonda hadharani..... Mzee Mkapa juzi alikemea utaratibu wa uteuzi wa viongozi wa umma akilenga uteuzi wa Makonda, mtu anayepiga wazee na kutukana viongozi.....
sie yetu macho tu
 

Attachments

  • Mtoto-wa-mwenzio.jpg
    Mtoto-wa-mwenzio.jpg
    27.1 KB · Views: 379
Ni wapi Warioba alisema hajapigwa? nakumbuka mara ya mwisho Warioba alisema wazi kapigwa na Makonda..... Mzee Butiku alimkemea Makonda hadharani..... Mzee Mkapa juzi alikemea utaratibu wa uteuzi wa viongozi wa umma akilenga uteuzi wa Makonda, mtu anayepiga wazee na kutukana viongozi.....
Kumbe mzee wako akiwa fisadi hata watoto mnakuwa mafisadi tena mafisadi wa akili.
 
Back
Top Bottom