Makonda apewa siku saba kesi ya Guninita

Makonda apewa siku saba kesi ya Guninita

Makonda-17April2015.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda

17th April 2015

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imetoa siku saba kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda, kuwasilisha utetezi wake dhidi ya kesi ya madai iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida, Mgana Msindai na Mwenyekiti CCM mkoa Dar es Salaam, John Guninita.

Kesi hiyo namba 68 ya 2015, Makonda alitakiwa kuwasilisha utetezi wake mahakamani jana, lakini wakili kupitia wakili wake, Lusiu Peter, ameomba Mahakama kumuongezea muda.

Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa amekubali ombi la utetezi na ametoa siku saba kwa Makonda kuwasilisha uetetezi wake hadi Aprili 23, mwaka huu.

Hakimu Riwa alisema kesi hiyo itatajwa Aprili 27,mwaka huu.

Katika kesi ya msingi, Msindai na Guninita wanaiomba mahakama hiyo kumuamuru Makonda awaombe msamaha na kumlipa kila mmoja Sh. milioni 100.

Wanadai fidia hiyo kutokana na maneno ya kuwadhalilisha yanayodaiwa kutolewa na Makonda kama Katibu Uhamasishaji na Chipukizi wa CCM katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Msindai na Guninita kupitia wakili wao, Benjamini Mwakagamba, wanaiomba Mahakama pamoja na mambo mengine itoe zuio la kudumu kwa Makonda asizungumze tena maneno ya kashfa wala kuyasambaza kama alivyofanya awali.

CHANZO: NIPASHE

Huyu Makonda si ndiye aliyetaka kumuhoji Gwajima kumbe na yeye anatakiwa kuhojiwa Kisutu. Laana ya kumpiga babu wa katiba mpya ya wananchi inazidi kumuandama.
 
Yaani na ww ni kilaza. Warioba kasema hajapigwa. Ww unasema warioba kapigwa. Mmh! Vp mm nikisema ww umelawitiwa.

Wewe ndo unalawitiwa na Makonda ndo maana unamtetea maana unajua ndo bwana wako!! Leo atakupa vya kukutosha kabisa!!
 
mahakani ndio mdudu gani?
kwanini una post mada nyingi nyingi, huoni unatukera kwa kutujazia saver na kutusumbua huku mada yenyewe haina kichwa wala miguu???

cc
mleta mada

Mkuu jifunze kupuuzia! Sio lazima usome kila kitu, mengine unayapita tu! Sasa ukisoma kila kitu utafanya kazi muda gani?!
 
mahakani ndio mdudu gani?
kwanini una post mada nyingi nyingi, huoni unatukera kwa kutujazia saver na kutusumbua huku mada yenyewe haina kichwa wala miguu???

cc
mleta mada

Badala ya kujadili hoja wewe unaruka na typing error! akili ndogo!
 
Huu uzi ndio ulinipa ban.watu wangapi hapo wamepingwa ban for name calling .huyu mod sijui anataka kunipa dada yake.




swissme
 
Unapewa cheo kwa Kumpiga Mzee Warioba ambaye anajenga hoja ya maneno.
Rais amekupa Ukuu wa wilaya kama Asante ya Ujasiri wako wa kupiga mzee yule, sijui kwenu kuna wenye mvi ?
Kwa ujinga wako wa kudhani ukileta noma zaidi cheo kitapanda basi unaamua kumtusi kila mtu ndani ya CCM.
Hivi hujauliza Bosi wako aliyekuteua alitukana watu wangapi mpaka akateuliwa kuwa Waziri?
Dogo unatumiwa hujui.
Wenyeviti wa CCM wanachaguliwa, wakuu wa wilaya wanapewa kishemeji na kishangazi.

Ukuu wa wilaya na mkoa ndivyo vyeo ambavyo Mpumbavu yeyote Tanzania anaweza kuvishika na kuongoza vizuri
kabisa.
Ukichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya usijione kwamba wewe ni JINIASI, Mmmm inawezekana UPUMBAVU wako ndiyo asili ya kuwa mkuu wa wilaya.

Hivi kwanini vijana Tanzania hawapendwi? au ndo umasikini unatusumbua? Hawa akina Guninita na Msindai wameshindwa kulea familia zao sasa wanashambulia watoto wa wenzao. Ipo haja ya kuwajenga kisaikologia watu kuondoka madarakani kwa amani na sio kusubiri kupigwa viti mikutanoni.
 
Wewe na mawazo yako hayo ya kuchukulia mambo kiimla utamjenga nani kisaikolojia?
Huyu Bwana mdogo Makonda alipompiga Mzee Warioba hiyo Saikolojia yako ilikuwa wapi.
Au hiyo wewe hukuiona.
Kama unapingana na mtu kwa hoja Ngumi za nini??
Kuna watu wanalipwa mamilioni kwa kupigana ngumi tu, na kamwe hawampigi mtu aliyewazidi hoja ili kumvuruga na kisha kuwekwa kwenye timu ya SPOILERS.
Vyama vyote vaya Siasa vinavyoendesha shughuli zake Kimafia ni lazima viwe na ATTACK DOGS
Makonda ni one of the attacks dogs wa CCM, Attack dog mashuhuri mwingine ni Mwigulu Nchemba ambaye sasa anakula matunda, Uwaziri.
Ndani ya CCM it pays kuwa Kijibwa cha Mashambulizi.
images

Who are the Masters of Makonda??

Sometimes you need to think critically.


Hivi kwanini vijana Tanzania hawapendwi? au ndo umasikini unatusumbua? Hawa akina Guninita na Msindai wameshindwa kulea familia zao sasa wanashambulia watoto wa wenzao. Ipo haja ya kuwajenga kisaikologia watu kuondoka madarakani kwa amani na sio kusubiri kupigwa viti mikutanoni.
 
Hawa mafisadi wanadhani mahakama inafanya kazi ya kusafisha mafisadi.

Nimefuatilia comment zako ni za kifisadi kabisa labda mumpige bomu asiwepo kwenye uchaguzi la sivyo labda mkimbie nchi baada ya kuapishwa huyo mnaemwita fisadi
 
Yaani na ww ni kilaza. Warioba kasema hajapigwa. Ww unasema warioba kapigwa. Mmh! Vp mm nikisema ww umelawitiwa.

Hapana jamani hivi Moderator wapo wapi haya ni MANENO MAKARI sana kwa nini tufike huku
 
siku zote ukishampiga mtu anayezidi umri wa baba yako lazima upate laana Paulo Makonda utavuna uliyoyapanda .
 
Last edited by a moderator:
siku zote ukishampiga mtu anayezidi umri wa baba yako lazima upate laana Paulo Makonda utavuna uliyoyapanda .

'Rudi msalabani Makonda' by Askofu Kakobe
 
Last edited by a moderator:
Vyeo v ya ukuu wa Wilaya na Ukuu wa mikoa ni VENT za MH Rais Pressure ikizidi huko juu.
Mahali ambapo Rais hutolea hewa chafu ili ajisikie vizuri.
Unakuwa mkuu wa wilaya wakati huo huo WALAYA WENYEWE huwajui wala hawakuhusu, kazi yako kubwa ni kupokea maagizo a kuyatekeleza bila hata kufikiri.
Ndiyo asili ya kuwaita SPOILERS.
President Vents.
 
Hawa wazee niliwah kuleta habar yao hapa kjpitia mwananchi newspaper wakimtaka Makonda aombe radhi,ni muda mrefu umepita nikajua yameisha kumbe walimaanisha.
Nakumbuka waliasema kuwa rais hajashauriwa vzuri kumteua Makonda.Ntaisaka ile Link

kwani washauri wa rais kwenye uteuzi huu ni kina nani mkuu??!! usikute ndio hao hao wa Makonda type!!!kesi ya fisi unampelekea mbwa mwitu!! teh teh teh !!!
 
Back
Top Bottom