Makonda apewa siku saba kesi ya Guninita

Makonda apewa siku saba kesi ya Guninita

Wakati wake umewadia....sasa Bwana DC ndiyo byebye.Nyamaume anamsubiri apandishwe kizimbani amfute kazi....byebye dogo mwenzako anakufuata.
 
Hapo bado mheshiwa huyu ajaanzisha yake

11124637_805786022847057_814749338_n.jpg
 
Taarifa yako haijakamilika. Je Makonda amepelekwa mahakama ipi na mashtaka yake ni yepi. Ni lini Makonda kapelekwa maHAKAMANI?

hujui kusoma! ? kuwa makini acha kukurupuka, siyo lazima uandike!
 
wakina Guninita ‘wamtia’ DC Makonda kortini - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ametakiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu kuwasilisha utetezi dhidi ya madai ya makada wawili wa CCM, John Guninita na Mgana Msindai kuwa aliwadhalilisha kwa kuwaita vibaraka wanaotumiwa kuharibu chama hicho kwa nguvu ya pesa.

Katika kesi hiyo ya madai Namba 68/2015,makada hao wawili wanataka walipwe fidia ya Sh100 milioni kila mmoja, Makonda awaombe radhi na mahakama itoe zuio la kudumu kwa kiongozi huyo wa Serikali kuwazungumzia.

Awali, Guninita, ambaye alikuwa mwenyeviti wa wa chama hicho mkoani Dar es Salaam, na Msindai ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoani Singida, walimtaka Makonda kuwaomba radhi kwa kutoa maneno ambayo walidai yanawadhalilisha, na kwamba asingefanya hivyo wangemfikisha mahakamani.

Mahakama ilikuwa imemtaka Makonda, ambaye anawakilishwa na Lusiu Peter, kuwasilisha utetezi wake leo lakini wakili huyo aliomba muda zaidi ili aandae majibu ya tuhuma hizo.

Kutokana na maombi ya wakili huyo wa Makonda, Hakimu Mkazi wa Kisutu, Hellen Liwa, anayeisikiliza kesi hiyo ya madai, alimtaka mkuu huyo wa wilaya ya Kinondoni kuwasilisha utetezi wake ifikapo Aprili 23 na kuahirisha kesi hiyo hadi Aprili 27 wakati itakapotajwa.

Katika kesi hiyo, Msindai na Guninita wanaiomba mahakama hiyo kumuamuru Makonda awaombe msamaha na kumlipa kila mmoja Sh100 milioni.

Msindai na Guninita wanadai kuwa Makonda aliwadhalilisha wakati akiwa katibu wa uhamasishaji chipukizi wa UVCCM kwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kuwaelezea makada hao kuwa ni vibaraka wanaotumiwa kuiharibu CCM kutokana na nguvu ya pesa.

JAMANI JAMANI TUACHE SIASA UCHWARA..........
 
Makonda huyu huyu aliyempiga mzee wa watu akalipwa u-Dc na mkubwa
 
Makonda sasa hivi yuko busy ana andaa shindano la kucheza dansi wilaya ya Kinondoni-childsh buf.fon
 
Kazi anayo mwaka huu. Waliokuwa wakimtuma wanasepa na kumwacha na mizigo ya lawama, laana na madeni yasiyo isha. Atavuna alichpkipanda
 
Taarifa yako haijakamilika. Je Makonda amepelekwa mahakama ipi na mashtaka yake ni yepi. Ni lini Makonda kapelekwa maHAKAMANI?

habari inajitosheleza na jina la mahakama limetajwa
 
Makonda sasa hivi yuko busy ana andaa shindano la kucheza dansi wilaya ya Kinondoni-childsh buf.fon

Hapo ndio ujinga wa Kikwete unajidhihirisha, angemchagua Super Nyamwela kuwa DC hii kazi kikwete amemtuma makonda kufanya ya kutafuta vipaji Nyamwela angeifanya vizuri
 
Alafu JK anamteua kuwa Mkuu wa Wilaya!
Kweli mambo mengine nikujidhalilisha kama Raisi na mtu binafsi.Kijana huyu tayari alikuwa amekweisha kosa sifa.
 
Unapewa cheo kwa Kumpiga Mzee Warioba ambaye anajenga hoja ya maneno.
Rais amekupa Ukuu wa wilaya kama Asante ya Ujasiri wako wa kupiga mzee yule, sijui kwenu kuna wenye mvi ?
Kwa ujinga wako wa kudhani ukileta noma zaidi cheo kitapanda basi unaamua kumtusi kila mtu ndani ya CCM.
Hivi hujauliza Bosi wako aliyekuteua alitukana watu wangapi mpaka akateuliwa kuwa Waziri?
Dogo unatumiwa hujui.
Wenyeviti wa CCM wanachaguliwa, wakuu wa wilaya wanapewa kishemeji na kishangazi.

Ukuu wa wilaya na mkoa ndivyo vyeo ambavyo Mpumbavu yeyote Tanzania anaweza kuvishika na kuongoza vizuri
kabisa.
Ukichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya usijione kwamba wewe ni JINIASI, Mmmm inawezekana UPUMBAVU wako ndiyo asili ya kuwa mkuu wa wilaya.
 
Ameshitakiwa kama MKUU wa WILAYA au kama MAKONDA ?
usikute na huyo wakili anayemteeta ni wa WILAYA/SEREKALI anatumia KODI zetu vibaya kwa maslahi yake binafsi.
 
Atakoma...anatukana na kuwapiga ngumi wazee wa nchi hii...!!!
 
Back
Top Bottom