Makonda anataka apange safu yake Arusha. Rais amempoteza

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
943
4,459
Unapokuwa kiongozi unayemtumia vyombo vya habari kudhalilisha watumishi wa umma unakuwa umemdhalilisha hata aliyekuteua.

Kinachotokea Arusha ni kumkwamisha Mhe. Rais, kwa sasa watumishi walio wengi wameweka mgomo. Kila analoelekeza hakuna anayelitekeleza badala yake wanasubiri aondoke na kamera zake na magari ya tours aliyolazimisha yaambatane naye.

Kwenye mikutano hata viongozi wa CCM wamegoma kushirikiana naye ; mkurugenzi ameshapishana naye kifikra na sasa hivi kila mtu anafanya awezavyo.

JPM alipoona udhalilishaji unakuwa mkubwa aliachana na huyu bwana mdogo. Sasa hivi anachofanya ni kutaka mawaziri na Mhe. Rais apeleke wale anaoona yeye anaweza kufanya nao kazi. Je, kila Mkuu wa Mkoa akiamua kuwachagua wa kushirikiana nao tutafika?
 
Unapokuwa kiongozi unayemtumia vyombo vya habari kudhalilisha watumishi wa umma unakuwa umemdhalilisha hata aliyekuteua...
kiongozi yeyote mwenye dhamana ya umma ni lazma kuwajibika kwa kazi na majukumu ulopewa kwa uwazi na kwa weledi mkubwa sana.

Au accountability na Transparency siku hizi ni kero na udhalilishaji?

unaelewa ni hatari sana kwa jamii kutokujua wala kuelewa inataka nini 🐒
 
Kiongozi sifa ya kwanza ni kuonyesha njia na unyenyekevu, hapo ana madaraka ya ukuu wa mkoa, anazurura na magari yote hayo, eti akakague ubadhirifu, wakati msafara wake ni ubadhirifu.

Anyway, ana kazi ya kusimamia ujenzi wa hoteli fulani na mru fulani, pamoja na ile ya Mrema iliyouzwa kwa mnada kwa mtu fulani. Kwa hiyo atakaa sana Arusha mpaka amalize hiyo project, labda baadae atatupwa mwanza akasaidie kukusanya kura za ukanda huo
 
Wakati wewe upo shwari kuna maelfu ya watanzania wanashida ambazo chanzo chake ni watumishi au wana kero na raia wenzao ambazo hazina hitimisho kwa uzembe wa mamlaka husika. Hiko ndio anachokionyesha Makonda.

Alipokuwa msemaji wa chama mmepiga majungu mpaka katolewa. Wakati ndani ya muda mfupi wa nafasi yake Makonda alikuwa anambadilishia upepo Samia. Mmeenda kuweka watu ambao hawajui kuongea na kadamnasi, majuzi jina la raisi limetajwa kwenye mkutano wa kutatua kero watu wamezomea.

Makonda kafika Arusha majuzi tu keshawapa polisi pikipiki 40, na anamjengea imani raisi mbele ya wananchi.

Mnapinga mambo wanayofanya wenzenu, wakati mkipewa kazi amuwezi kuonyesha matokeo chanya. Mama watu kawatafutia hela kweli hakuna kinachoonekana watu wamezila karibu zote.

Ni sampuli ya watu wa aina hii ndio mlioharibu uraisi wa Samia aonekane wa hovyo, amtaki mabadiliko mnataka kulinda status yenye culture ya uzembe, kutowajibika na wizi. Wakati utaratibu huo unaumiza maskini ambao ukweli wenyewe wamemchoka huyo mama.
 
Naona sindano imekuingia vizuri , mpaka unaongea vitu visivyo vya kweli. Yaan unapayukapayuka kama mgonjwa wa malaria. Sindano ya makonda inachoma kweli kweli.

Tulia Makonda anachoma kwa siku sita hapo Arusha. Tulia sindano iingie vizuri. Ukimaliza kupokea doz ya hiyo sindano nenda kawambie hao watumishi waache wizi wa pesa za serikali.
 
kiongozi yeyote mwenye dhamana ya umma ni lazma kuwajibika kwa kazi na majukumu ulopewa kwa uwazi na kwa weledi mkubwa sana.....

Au accountability na Transparency siku hizi ni kero na udhalilishaji?

unaelewa ni hatari sana kwa jamii kutokujua wala kuelewa inataka nini 🐒
Jamii inataka katiba mpya, sio kiki za muhalifu.
 
Mimi siyo Mwana-ccm kabisa ila mleta mada kwa taarifa yako anachofanya Makonda itakuwa kilio kwa wapinzani kama hatutakuja na strategy mbadala ya kujieleza kwa wananchi.

Hakuna kitu mwenye shida anachokifurahia kama kusikilizwa kwa shida yake, hata kama hatatekelezewa anachokihitaji ila ameeleza na kusikilizwa, moyo wake unaanza kuambatana na msikilizaji.......
 
Back
Top Bottom