Makonda anafanya kazi nzuri, ila awe makini na kinywa chake

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
6,049
8,411
Madudu anayoyaibua yanawaumbua watangulizi wake na hata "maRC"wa mikoa mingine. Kwa sasa anajulikana nchi nzima, lakini kuna watu hawayajui hata majina ya wakuu wa mikoa yao.

Mbali na kuwa anayoyafanya yana maslahi kwa umma, si wote, hasa watawala wenzake, watakaomfurahia.

Naamini naye ana account humu. Ujumbe utamfikia.

Ninayataja baadhi ya makosa aliyoyafanya ili asiyarudie.

1. Kejeli kwa wanawake

Kada mwenzake wa Chama alimtuhumu kuwa anawadhalilisha wanawake. Bila shaka tuhuma zimeibukia pale alipomwambia Eng. wa kike asiongee kama anayechumbiwa kwa sababu yeye ana mke tena mzuri. Hapo alikosea. Hakupaswa kumjibu hivyo. Ni sahihi kukemea pale inapobidi, lakini kukejeli na kuainisha iwe ni mwiko.

2. Kupigiwa magoti na Mkurugenzi wa jiji la Arusha

Nionavyo, asingepaswa kuliweka hilo wazi. Maadam huyo bwana alimfuata faragha katika jitihada za kuokoa kibarua chake, asingeueleza uma yote yaliyotendeka ofisini wakiwa wawili. Hakukuwa na umuhimu wa kueleza kuwa mkurugenzi alimpigia magoti. Kiongozi hapaswi kusema kila kitu hasa kama hakina maslahi kwa anaowaongoza.

3. Mawaziri wanaomtukana Rais

Labda kama mfumo uliamua kutumia mbinu ya "gun boot diplomacy" kuwanyamazisha wapinzani wa Rais Samia walio Serikalini kwa kumtumia Makonda.

Kinyume na hapo, alikosea. Alipaswa kuliwasilisha suala husika ama kwa bosi wake (Rais) au Chama chake au vyombo mamlaka zingine zinazohusika. Alichokifanya Monduli kilitafsiwiriwa kuwa alikuwa akitafuta umaarufu, na pengine, kujipendekeza kwa Rais Samia.

4. Kutabiriwa Urais

Inawezekana ana ndoto ya kuja kugombea Urais wa JMT, na si kosa akifanya hivyo. Lakini anapaswa kujihadhari ili wanaokitamani hicho kiti wasione anajitengenezea mazingira ya kujiimarisha katika hilo. Hawatachelewa kumtengenezea zengwe la kumkwamisha. Kitendo cha baadhi ya watu kuonesha kuwa wanatamani awe Rais wa JMT kinamwongezea maadui.

Kuna watu wamekuwa wakijiandaa kwa hiyo nafasi tokea 2010. Hawatamfurahia hata kidogo, na ikizingatiwa kuwa miongoni mwao ni watu wenye ushawishi Serikalini, wanaweza kutengeneza mkakati wa kumdhibiti. Kama ana nia ya kuja kugombea, kwa sasa anapaswa kuigiza kutokuwa na uhitaji huo. Huo ni kwa usalama wale mwenyewe na ndoto yake pia. Nafikiri anazijua fitna za wanasiasa wa Tanzania, hasa wa Tanganyika.

Pamoja na mapungufu yake kama ilivyo kwa binadamu wengine, Makonda anafanya kazi nzuri. Leo hii kungeitishwa kura ya kumchagua RC bora, Makonda angeibuka kidedea.

Kama atajitahidi kujizuai asiongee kwa mihemko, ataweza kufanya makubwa zaidi.

Bila shaka anaweza kufanya hivyo.

Ukimwangalia Makonda wa miaka ya nyuma akiwa RC wa Dar Es Salaam ni tofauti na WA sasa RC wa Arusha. Makonda wa Arusha anaonekana "amekua". Hata hivyo, bado anapaswa kukua zaidi ya hapo alipofikia.
 
Mkurugenzi naye farasi tu,yaani zee jitu zima linampigia mkolomije magoti alafu mkolomje kaja kulidhalilisha.Hata mke wake kama alisikia atamyima pochi miezi sita ajifunze kukaza.Mkolomije endelea kupiga kwenye mshono mpaka kieleweke.
 
😂 😂 😂 😂
Naona unampigia tena gitaa la rhythm na ka muziki ka kwenye massage
 
Madudu anayoyaibua yanawaumbua watangulizi wake na hata "maRC"wa mikoa mingine. Kwa sasa anajukikana nchi nzima, lakini kuna watu hawayajui hata majina ya wakuu wa mikoa yao.

Mbali na kuwa anayoyafanya yana maslahi kwa uma, si wote, hasa watawala wenzake, watakaomfurahia.

Naamini naye ana account humu. Ujumbe utamfikia.

Ninayataja baadhi ya makosa aliyoyafanya ili asiyarudie.

1. Kejeli kwa wanawake

Kada mwenzake wa Chama alimtuhumu kuwa anawadhalilisha wanawake. Bila shaka tuhuma zimeibukia pale alipomwambia Eng. wa kike asiongee kama anayechumbiwa kwa sababu yeye ana mke tena mzuri. Hapo alikosea. Hakupaswa kumjibu hivyo. Ni sahihi kukemea pale inapobidi, lakini kukejeli na kuainisha iwe ni mwiko.

2. Kupigiwa magoti na Mkurugenzi wa jiji la Arusha

Nionavyo, asingepaswa kuliweka hilo wazi. Maadam huyo bwana alimfuata faragha katika jitihada za kuokoa kibarua chake, asingeueleza uma yote yaliyotendeka ofisini wakiwa wawili. Hakukuwa na umuhimu wa kueleza kuwa mkurugenzi alimpigia magoti. Kiongozi hapaswi kusema kila kitu hasa kama hakina maslahi kwa anaowaongoza.

3. Mawaziri wanaomtukana Rais

Labda kama mfumo uliamua kutumia mbinu ya "gun boot diplomacy" kuwanyamazisha wapinzani wa Rais Samia walio Serikalini kwa kumtumia Makonda.

Kinyume na hapo, alikosea. Alipaswa kuliwasilisha suala husika ama kwa bosi wake (Rais) au Chama chake au vyombo mamlaka zingine zinazohusika. Alichokifanya Monduli kilitafsiwiriwa kuwa alikuwa akitafuta umaarufu, na pengine, kujipendekeza kwa Rais Samia.

4. Kutabiriwa Urais

Inawezekana ana ndoto ya kuja kugombea Urais wa JMT, na si kosa akifanya hivyo. Lakini anapaswa kujihadhari ili wanaokitamani hicho kiti wasione anajitengenezea mazingira ya kujiimarisha katika hilo. Hawatachelewa kumtengenezea zengwe la kumkwamisha. Kitendo cha baadhi ya watu kuonesha kuwa wanatamani awe Rais wa JMT kinamwongezea maadui.

Kuna watu wamekuwa wakijiandaa kwa hiyo nafasi tokea 2010. Hawatamfurahia hata kidogo, na ikizingatiwa kuwa miongoni mwao ni watu wenye ushawishi Serikalini, wanaweza kutengeneza mkakati wa kumdhibiti. Kama ana nia ya kuja kugombea, kwa sasa anapaswa kuigiza kutokuwa na uhitaji huo. Huo ni kwa usalama wale mwenyewe na ndoto yake pia. Nafikiri anazijua fitna za wanasiasa wa Tanzania, hasa wa Tanganyika.

Pamoja na mapungufu yake kama ilivyo kwa binadamu wengine, Makonda anafanya kazi nzuri. Leo hii kungeitishwa kura ya kumchagua RC bora, Makonda angeibuka kidedea.

Kama atajitahidi kujizuai asiongee kwa mihemko, ataweza kufanya makubwa zaidi.

Bila shaka anaweza kufanya hivyo.

Ukimwangalia Makonda wa miaka ya nyuma akiwa RC wa Dar Es Salaam ni tofauti na WA sasa RC wa Arusha. Makonda wa Arusha anaonekana "amekua". Hata hivyo, bado anapaswa kukua zaidi ya hapo alipofikia.
Umechambua vizuri, ila hili la Urais halitamki yeye, linatamkwa na raia anaowafurahisha.

Kwa utendaji wake maridhawa, raia mikoa yote kwa sasa wanamfuatilia Rc wa Arusha kuliko wanavyolifuatilia Bunge ama wanavyosikiliza hotuba ya Rais.

Hakika uchambuzi wako ninauunga mkono juu ya kujidhibiti na kauli zake anapokuwa kapanda jaziba zitokanazo na maudhi ya mafisi.
 
Wanasema, mbinu mojawapo ya vita ni kujifanya uko mbali ilhali upo karibu sana na kujifanya upo jirani mno wakati upo mbali sana. Kwa kukaa kwake kimya "alipotamkiwa" hilo hadharani kutawaweka katika tahadhari wale wote wanaokitamani hicho kiti.

Unawajua wanasiasa lakini?

Wengine wapo tayari kufanya lolote, hata kama ni ukatili, ili tu watimize azma yao.

Busara ni kujifanya hana "time" na Urais hata kama anuhitaji, hadi hapo muda muafaka utakapowadia.

Angefanya kama JPM. Yeye hakuwahi kuweka wazi kuwa anataka Urais. Alitarajiwa kuwa atakuwa mjenzi wa mabarabara siku zote hivyo hakuonekana tishio kama ilivyotukia kwa akina Lowassa.

Ni ushauri tu lakini. Ana haki ya kuupokea au kuutupilia mbali.
 
Madudu anayoyaibua yanawaumbua watangulizi wake na hata "maRC"wa mikoa mingine. Kwa sasa anajulikana nchi nzima, lakini kuna watu hawayajui hata majina ya wakuu wa mikoa yao.

Mbali na kuwa anayoyafanya yana maslahi kwa umma, si wote, hasa watawala wenzake, watakaomfurahia.

Naamini naye ana account humu. Ujumbe utamfikia.

Ninayataja baadhi ya makosa aliyoyafanya ili asiyarudie.

1. Kejeli kwa wanawake

Kada mwenzake wa Chama alimtuhumu kuwa anawadhalilisha wanawake. Bila shaka tuhuma zimeibukia pale alipomwambia Eng. wa kike asiongee kama anayechumbiwa kwa sababu yeye ana mke tena mzuri. Hapo alikosea. Hakupaswa kumjibu hivyo. Ni sahihi kukemea pale inapobidi, lakini kukejeli na kuainisha iwe ni mwiko.

2. Kupigiwa magoti na Mkurugenzi wa jiji la Arusha

Nionavyo, asingepaswa kuliweka hilo wazi. Maadam huyo bwana alimfuata faragha katika jitihada za kuokoa kibarua chake, asingeueleza uma yote yaliyotendeka ofisini wakiwa wawili. Hakukuwa na umuhimu wa kueleza kuwa mkurugenzi alimpigia magoti. Kiongozi hapaswi kusema kila kitu hasa kama hakina maslahi kwa anaowaongoza.

3. Mawaziri wanaomtukana Rais

Labda kama mfumo uliamua kutumia mbinu ya "gun boot diplomacy" kuwanyamazisha wapinzani wa Rais Samia walio Serikalini kwa kumtumia Makonda.

Kinyume na hapo, alikosea. Alipaswa kuliwasilisha suala husika ama kwa bosi wake (Rais) au Chama chake au vyombo mamlaka zingine zinazohusika. Alichokifanya Monduli kilitafsiwiriwa kuwa alikuwa akitafuta umaarufu, na pengine, kujipendekeza kwa Rais Samia.

4. Kutabiriwa Urais

Inawezekana ana ndoto ya kuja kugombea Urais wa JMT, na si kosa akifanya hivyo. Lakini anapaswa kujihadhari ili wanaokitamani hicho kiti wasione anajitengenezea mazingira ya kujiimarisha katika hilo. Hawatachelewa kumtengenezea zengwe la kumkwamisha. Kitendo cha baadhi ya watu kuonesha kuwa wanatamani awe Rais wa JMT kinamwongezea maadui.

Kuna watu wamekuwa wakijiandaa kwa hiyo nafasi tokea 2010. Hawatamfurahia hata kidogo, na ikizingatiwa kuwa miongoni mwao ni watu wenye ushawishi Serikalini, wanaweza kutengeneza mkakati wa kumdhibiti. Kama ana nia ya kuja kugombea, kwa sasa anapaswa kuigiza kutokuwa na uhitaji huo. Huo ni kwa usalama wale mwenyewe na ndoto yake pia. Nafikiri anazijua fitna za wanasiasa wa Tanzania, hasa wa Tanganyika.

Pamoja na mapungufu yake kama ilivyo kwa binadamu wengine, Makonda anafanya kazi nzuri. Leo hii kungeitishwa kura ya kumchagua RC bora, Makonda angeibuka kidedea.

Kama atajitahidi kujizuai asiongee kwa mihemko, ataweza kufanya makubwa zaidi.

Bila shaka anaweza kufanya hivyo.

Ukimwangalia Makonda wa miaka ya nyuma akiwa RC wa Dar Es Salaam ni tofauti na WA sasa RC wa Arusha. Makonda wa Arusha anaonekana "amekua". Hata hivyo, bado anapaswa kukua zaidi ya hapo alipofikia.
Si kejeli kwa wanawake bali anakiburi cha madaraka
 
Back
Top Bottom