Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Kiroho Mkonda alikuwa anafanya upatanisho, hii inawezekana tu kama dhamira yako ni nyeupe na hamna element za visasi kabisa.
Hakuna upatanisho wa kiroho kati ya nafsi hai na iliyokufa.
Pataneni wakati mngali hai,maana upatanisho wa kweli ni maridhiano ya pande mbili zilizohai
All in all...Hii ni ajali kazini!!Ya Kaisari hubaki kwa Kaisari
 
ujumbe unaokwenda kwenye jamii ni kwamba bwana makondakta aache UNAFIKI. mtu amesababisha kifo cha mpendwa wao halafu anaenda kuwapo mikono ya kinafiki ili iweje?
Labda we ndo umesababisha
 
Hakuna upatanisho wa kiroho kati ya nafsi hai na iliyokufa.
Pataneni wakati mngali hai,maana upatanisho wa kweli ni maridhiano ya pande mbili zilizohai
All in all...Hii ni ajali kazini!!Ya Kaisari hubaki kwa Kaisari
No sina maana na marehemu bali na familia ya Marehemu, "he wanted to heal their souls"
 
Mpuuzi tu..sasa kwa kumchunia inasaidia nini?baba yake hakuwa muadilifu,hilo halina ubishi.kote alikopita alikuwa analaumiwa.angekuwa muungwana angemwambia baba yake aache ubadhilifu..mjinga tu.kwanza hata makonda amefanya ubinadamu tu kwenda msibani.
Ni Kweli, Lakini Ufisadi aliokuwa amefanya Ulishabainika, Na Taarifa za Tukukuru, za Bunge zilionyesha hivyo, Lazima angewajibishwa na Na Jiji Linaloongozwa na Ukawa. Alichofanya Makonda Ni kukimbilia mbio kueleza hadharani ili ionekane yeye ndiye aliyegundua madudu ya Kebwe. Hakuwa na Nia Nzuri kama mnavyofikiri. Ni mkakati wa Kufagia nyumba haraka ili mgeni asije akachukua fagio! Uchafu ambao jana tu Uliukalia na kuulalia! Sasa Nijue Kufagia huko ni chuki ya uchafu au Ni hadaa kwa Mgeni?
 
Nimekuelewa Mkuu...Ni kweli
Maana wanasema tusameheane 7X70,lkn kumbuka "shujaa" wa kwanza mwanaume kwa Mtoto wa kike huwa ni baba yake
Wanawake wapo "emotional" sana,hii kwa binti ni kawaida sana kama alivyosema ndugu yangu UncleBen
Ni kweli kabisa Mkuu , Watoto wa kike mara nyingi wanafikiri kuwa wanume wote wana tabia kama za baba zao, Wakiolewa ndio huona tofauti.
 
hakukuwa na ulazima wa makonda kwenda pale

Hapa issue sio kuhusu wizi wa marehemu...hapa ni kuhusu hisia za wafiwa...they deserved respect
Tokea hapo mwanzo palipoanza kuwa na contradictory statements kutoka kwa wana familia kuhusu serekali kushiriki kwenye mazishi, ilionesha wazi kuwa wako walo support na wako walokuwa hawa support.Makonda should have known better, haikuwa na lazima yeye kwenda pale, angweza ku avoid haya mambo. It was a bad judgment from him.
 
Ni kweli kabisa Mkuu , Watoto wa kike mara nyingi wanafikiri kuwa wanume wote wana tabia kama za baba zao, Wakiolewa ndio huona tofauti.
Na mara nyingi mabinti waliolelewa na Wababa "smart" hupata shida sana katika ndoa zao,maana hutaka kuwalinganisha waume zao na tabia za baba zao
Binti anakumbuka jinsi Mama alivyokuwa "well treated" na baba yake,anaona mbona huyu wangu hafanyi kama baba alivyokuwa anafanya kwa Mama??

Ndio maana unakuta kutwa kucha binti anasema "Aaa yani baba alikuwa anamfanyia Mama hivi na vile"
Ukizingatia Baba kama Kabwe,alikuwa anawalea watoto wake kwa maisha safi,shule unaenda kwa amani,hela ya matumizi,hupati shida uwapo shule au chuo nk

Lazima aumie,asononeke na hasa akiona baba anasemwa hadharani na "mtoto" kama Makonda.Maana Mzee anapokuwa anapiga madili hasemi kuwa hizi ni hela za madili.

Damu nzito kuliko maji,niliwahi kukaa na jamaa baba yake ni mlevi sana,lkn alikuwa hakosi kuwalea watoto wake vizuri,kuna siku tunapita sehemu tukakuta watu wanapiga kelele eneo la Bar,ikabidi tupite kutazama,kufika pale tukakuta baba wa jamaa amelewa chakari,kajikojolea na amelala fofofo
Barmaid anamvuta kumuamsha Mzee wafunge Bar...huku akitoa maneno makali na kumzaba makofi.Damu nzito kuliko maji,Jamaa alitembeza kichapo kwa bar maid na waliokuwa wanamgasi Mzee,akamchukua mzee kwenye Tax hadi home

Japo kiukweli mzee alichokuwa kafanya hakikuwa sahihi,lkn mtoto alipatwa na "damu nzito" akamsaidia.Binti yupo sahihi
 
Jaman mambo mengine sio ya kupost humu, kwanza unapoandika vile ni dhahiri kuwa umefurahishwa na kitendo cha huyo binti, pia mi sioni kosa la makonda kusema makosa na ubadhilifu wa kabwe uliopelekea mpaka kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pia ieleweke kuwa kazi ya kutumikia umma huhitaji mhusika awe na uadilifu kwa umma.
Kabwe amefanya kazi kama mkurugenzi kwa mkoa wa mwanza, mbeya na dar lakini udhaifu mkubwa ulionekana ukiambatana na ubadhilifu, kusimamishwa kazi kusiwe sababu ya kumuona kuwa alikuwa mwema mno kiasi cha kumuona makonda kama kihelehele kwani naamini aliyafanya yote hayo kwa faida ya wanadaresalaam wote hata watanzania kwa ujumla.
Kila kifo kina sababu zake, kama inasemekana tayari alikuwa mgonjwa, je haikupaswa kumsimamisha kazi kisa mgonjwa kwa kuhofia atafariki? Tuacheni unafiki wa kuwa vigeugeu wasioeleweka, baadhi mlilalamika kuwa marehemu alikuwa tatzo leo tena lawama kwa makonda?
R.I.P KABWE
Mimi Sipendi Ufisadi hata Kidogo Ila Nimefurahi sana, Kwanza Ningekuwa Mimi Ningempa mkono mtakatifu! Makonda hakumtaja Kabwe Mbele ya JPM kwa Kuchukia Ufisadi, alitaka SIFA, Ni sawa na Kuona Mzoga wa Tembo unakimbia Kuwaita Wanakijiji na Kuwaambia angalieni tembo Nimeua sasa hivi, wakati walimpita akiwa amelala pale kila siku. Nani hapa ataniambia kwa taarifa za Takukuru, Bunge na Kadhalika JPM alikuwa hajui Ufisadi wa Kabwe mpaka atajiwe na Makonda. Na isitoshe kwani Makonda hamwonagi Rais au hawezi kuwasiliana naye Kiofisi Kumpa Taarifa hiyo Mpaka aseme kwenye Ufunguzi wa Daraja. Wewe Huoni Hiyo ilikuwa na Nia ya Kutaka sifa. SAFI SANA BINTI YANGU, Namfananisha na Rosa Parks
 
N
Ni ujinga tu wa huyu makonda

Anajua fika kwenda kwake pale anawaongezea wafiwa maumivu

Kiherehere cha nini kujipeleka...si angeenda mkuu wa wilaya

Huu ni ukosefu wa Ubinadamu

Lile lilikuwa suala la kifamilia....Alitakiwa tu kutumia common sense

Ni kama alikwenda kuwatambia kwamba amewakomesha! Kweli he should have stayed away kutokana na sensitivity ya tukio na jambo alilolifanya, ni kweli common sense is not always common!
 
Poleni kwa msiba family ya Kabwe na imani mungu atamlaza mahala pema peponi ..Ila hakuna alie mkamilifu kila mtu ana makosa yake Makonda alikosea na Marehemu alikosea Mtoto amekosea na kuna makosa kwenye mahojiano kwenye jf na hata mimi navyoandika hapa huenda nakosea,. Je ungelikuwa wewe ungefanyaje baada ya kutokewa na msiba kama huyo dada hapo
 
mkuu huoni kama upinzani umegeuka upande kuelekea kule ambako haukuwahi kuelekea siku za nyuma.
Naichukia ccm kwa sababu ya ufisadi ila naanza kuichukia tena chadema. Kweli leo chadema wanalaumu kabwe kutumbuliwa, wakati walimuimba wakati wote kuanzia bungeni, nusura ampoke Wenje ubunge 2010, leo wanasikitika kutumbuliwa kwake. Dah wamenisikitisha sana.
 
Hapana...Lakini just fikiria kibinadamu mzazi wako ndio amefariki alafu anakuja mtu aliyeamua kuonesha chuki za wazi kabisa na mzazi wako...eti anajipendekeza msibani kuwa anajali

Huo ni ujinga na Unafiki

Pia kumbuka watoto wa kabwe pia wana maumivu
Mbona mnatuhumu Makonda kama muuaji jamani acheni hizo hisia kuwa 100% kifo ni sababu ya kutumbuliwa.Makonda yuko sahihi jamani ametimiza majukumu ya kazi yake na anajua wajibu wake ndio maana hata dhamiri yake haimshtaki kwenda msibani.Kwani mtoto wako akikosea ukampa adhabu unamchukia na kumtenga?Ninavyomuelewa makonda ni mtu wa watu.Pia kwa rais kumtuma mwakilishi si sababu anaogopa kwenda ila ana majukumu mengine mbona ni kawaida sana kutuma wawakilishi.
 
Hivi Hamjaona watu wanaotaka Sifa Kupindukia, mpaka yupo tayari Kuhatarisha Maisha, Nimeona watu wanaopiga Busu Cobra, Nimeona Watu wanaingiza Vichwa vyao vinywani mwa mamba. Wengi ni kwa Kutaka sifa na Wote hawa Makonda amewazidi!
dsc8005.jpg
The Likes of Makonda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom