Makombora ya Hizbullah ya Lebanon yapigangome za kijeshi za Israel

LINGWAMBA

JF-Expert Member
Sep 30, 2023
421
946

  • Makombora ya Hizbullah ya Lebanon yapiga ngome za kijeshi za Israel
Wapiganaji wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon wameshambulia kwa makombora vituo na ngome za kijeshi za Israel kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kusambaratisha mfumo wa kamera za usalama wa utawala huo haramu.

Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya al-Mayadeen, wanajihadi wa Hizbullah jana usiku walishambulia kwa maroketi mazito kambi tano za kijeshi za Israel katika eneo la Al-Jalil, yaliyovurumishwa kutoka kusini mwa Lebanon.

Sauti za ving'ora zimesikika kwa saa kadhaa kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kupachikwa jina bandia la Israel, kutokana na wimbi la makombora yaliyolenga ngome hizo za kijeshi za Wazayuni.

Kwa mujibu wa al-Mayadeen, Hizbullah imeharibu kikamilifu mfumo wa kamera za usalama wa utawala huo haramu uliosimikwa majuzi, kwa kuupiga kwa kombora la ardhini hadi ardhini la Falaq-1 katika mji wa Zar'it karibu na mpaka wa Lebanon.

Aidha wanajihadi hao wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah usiku wa kuamkia leo walishambulia kwa makombora kambi za kijeshi za utawala wa Kizayuni za Hunin Castle mjini Margaliot, Hanita, Avivim, Doviv , Metula na Shlomi karibu na mpaka wa Lebanon.
4c69f67c1efba72fvq7_800C450.jpg

Wanajihadi hao wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon siku chache zilizopita walitibua uvamizi wa kijeshi wa Israel na kulisababishia hasara kubwa jeshi la utawala wa Kizayuni katika mji wa Zar'it karibu na mpaka wa Lebanon, kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu.

Ngome za utawala huo ghasibu zinaendelea kulengwa kwa maroketi na makombora ya kundi hilo la muqawama, likiwa ni jibu kwa mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Wazayuni katika Ukanda wa Gaza.
 
Umeiandika hii habari kishabiki! Lakini taarifa zilizopo IDF inaweza kuishambulia Labanoni kusini ili kuwafurusha wapiganaji wa Hezibollah!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom