Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimetangaza kuwa, wakazi wa miji na vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyoko kwenye mpaka wa Lebanon wanakimbia kwa umati kwa namna ambayo haijawahi kutokea katika historia ya Israel sambamba na kuendelea Hizbullah ya Lebanon kuyapiga kwa makombora maeneo tofauti ya utawala wa Kizayuni kama sehemu ya kuwaunga mkono wananchi wa Ghaza.
Televisheni ya al Mayadeen imevinukuu vyombo vya habari vya Kizayuni vikitangaza kuwa, miji na vijiji vyote vya eneo la al Khalil al A'laa pamoja na kituo kikuu cha komandi kuu ya kijeshi ya Israel wamekimbia eneo hilo kwa kuhofia mashambulizi ya wanamapambano wa Kiislamu. Vyombo hivyo vya Israel vimesema, hadi hivi sasa haijawahi kutokea wimbi kubwa kiasi hiki cha Wazayuni kukimbia maeneo yao tangu ulipounda utawala pandikizi wa Kizayuni zaidi ya miaka 75 iliyopita.
Vyombo hivyo vya Kizayuni vimesema, tangu Hizbullah ya Lebanon ilipoanzisha mashambulizi ya kuwaunga mkono wananchi wa Ghaza, makumi ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni karibu na mpaka wa Lebanon vimebaki vitupu bila ya watu. Lakini kuondoka kikamilifu watu wote katika miji ya eneo la al Khalil al A'laa ni jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia yote ya utawala wwa Kizayuni wa Israel.
Huku hayo yakiripotiwa, harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeendelea kuyapiga kwa makombora maeneo tofauti ya Israel ikiwa ni kuwaunga mkono wanamapambano wa Palestina wanaendesha mapambano ya kishujaa kwenye Ukanda wa Ghaza pamoja na wananchi madhlumu lakini wenye nguvu na subira kubwa wa ukanda huo.
Taarifa zinasema kuwa, jana pia Hizbullah iliitwanga kwa makombora kambi ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni huko kaskazini mwa ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel.
Televisheni ya al Mayadeen imetangaza katika ripoti yake nyingine kwamba, Hizbullah ya Lebanon imejibu jinai za Israel za kushambulia hospitali za Ukanda wa Ghaza kwa kuipiga kwa makombora kambi ya kijeshi ya al Asi ya utawala wa Kizayuni, kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni