Makocha kumi bora kuwahi kufundisha mpira wa miguu Tanzania 1990-2022

Unaonekana unapenda sana mpira

Kama binti ningependa kujua uliingiaje kwenye mpira

Je unapenda mpira kweli au unapenda timu?
Je unafatilia mechi nyingi au unafatilia mechi za timu yako tu ikicheza

Km unanafasi tukualike kwenye media
Basi tufanye uzi ubatilishwe tuuu
 
Moja kati ya Makocha WAKUBWA.

Wenye Elimu zaidi kuwahi kufundisha Tanzania ni PIER RECHANTE.

PATRIC RECHANTE ALIONDOKA HOVYO SANA.
 
Wafuatao kwa maoni yangu ndio makocha bora kwa kipindi chote cha uhai wa Tanzania na sio kama alivyotaka mleta nyuzi yaani kuanzia 1990.
  • Victor Stanculescu (Romanian) – Young Africans Coach 1971 to 1974, huyu ndiye kocha bora kwangu kuwahi kufundisha kandanda hapa nchini. Aliipa Yanga ubingwa mara tatu 1971, 1973 na 1974. Alikuza kipaji cha mchezaji bora kuwahi kutokea Tanzania Sunday Manara, lakini kama haitoshi yeye ndiye mwanzilishi wa timu za watoto, aliunda kikosi cha Yanga Kids kwa watoto alio watoa mitaani na kuwafundisha soka na baadaye wakaja kuwa nyota wakubwa sio Tanzania tu hata barani ulaya. Nyota hao ni Juma Pondamali, Jaffar Abdulrahman, Mohammed Mkweche, Mohammed Rishard Adolph, Bona Max, Gordian Mapango, Mohammed Yahya “Tostao”, Kassim Manara na wengine. Kasim Manara na Tostao baadaye walicheza kwa mafanikio nchini Austria, sema wakati huo hatukua na mitandao ya kutupa taarifa kama kipindi cha kina Samata. Victor miaka ya 2000 mwanzoni alikuja tena Tanzania kama kocha wa Taifa stars, awamu hii akiwa mmarekani lakini alikaa miezi miwili tu akaondoka mwenyewe baada ya kuona uswahili mwingi.
  • Paul West Gwivaha (Mtanzania) – Simba SC 1974 na Taifa Stars Coach 1973. Huyu nampa no 2, alikuwa ni kocha wa Taifa Stars, lakini FAT waliipa Simba kocha huyo aifundishe katika kugombea kombe la klabu bingwa 1974. Nakumbuka mwaka 1973 akiwa kocha wa Taifa Stars Tanzania ilifuzu kushiriki michuano ya All Africa Games siyo AFCON iliyofanyika Lagos Nigeria 1973. Baada ya kushiriki mashindano hayo Wachezaji wawili wa Taifa Stars Maulid Dilunga na Omar Mahadhi Bin Jabir walichaguliwa timu ya Africa iliyowakilisha katika michuano ya mabara iliyofanyika Mexico 1973. Akiwa kocha wa Simba 1974, aliiwezesha Simba kufika hatua ya nusu fainali klabu bingwa ya Africa, hatua ambayo haijafikiwa na klabu yoyote hapa nchini. Simba ilikuwa na uwezo wa kuchukua kombe mwaka huo, lakini walifanyiwa vurugu nyingi na klabu ya Mehalla Al kubra ya Misri, ikiwemo kipa wa Simba athumani Mambosasa kuvamiwa na mashabiki na kutishiwa kisu, Simba ilitolewa kwa penalty. Wakati penalty zikipigwa washabiki wa Mehalla walikuwa nyuma ya goli wakimzodoa Mambosasa. Chini ya Gwivaha 1974, Simba walikuwa wakicheza kandanda safi sana, Gwivaha alifanikisha kupandisha viwango vya wachezaji kama Kibadeni, Saad Ally na Mambosasa. K sana atika hatua ya robo fainali Simba iliitoa timu tishio barani Africa wakati huo Accra Hearts of Oak ya Ghana iliyokuwa na washambuliaji hatari sana wakati huo kama Mama Acquah na mohammed Pollo.
Makocha 8 waliobakia ambao kama nitapata muda nitaeleza sifa na mafanikio yao

  • Abdallah Kibadeni
  • Joel Bendera
  • Dragan Popadic
  • Tambwe Leya
  • Nabby Camara
  • James Siang’a
  • Rudy Gutenderndoff
  • Gomez
Asante kwa kuleta taarifa nzuri. Niliepuka kuandika waliokuwepo kabla ya 1990 maana sina details za kutosha. Hope utapata muda uandike kuhusu hao wengine ili tuwafahamu zaidi.
 
Back
Top Bottom