Mkwasa"master" Gwiji la mpira ndani na nje ya uwanja,mwanafalsafa wa mpira wa kushambulia muda wote

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
MKWASA"MASTER" GWIJI LA MPIRA NDANI NA NJE YA UWANJA,MWANAFALSAFA WA MPIRA WA KUSHAMBULIA MUDA WOTE.

Leo 12:15pm,19/01/2020

Charles Boniface Mkwasa "Master" beki bora kuwahi kutokea na kiungo bora wa muda wote katika mpira nchini Tanzana,ndiye Mchezaji Bora chipukizi wa Tanzania mwaka 1975 na Mchezaji Bora wa Tanzania mwaka 1981.

Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ Nahodha wa zamani wa Taifa Stars,Kocha wa kwanza Mzalendo wa Taifa Stars,Ndiye kocha aliyepata kurejesha furaha kwa Watanzania,

Charles Boniface Mkwasa alizaliwa Aprili 10 mwaka 1955 mjini Morogoro, alipata elimu yake ya Msingi na sekondari mkoani Morogoro ambapo alikuwa akionyesha kandanda safi wakati mechi za madarasa hata shule na shule kwenye iliyokuwa Umiseta na Umitashumta.

Tumepata kushuhudia vipaji vizuri sana kutoka kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari,kiukweli Umitashumta na Umiseta ulileta vipaji vingi kwenye michezo, vijana waliendelezwa na walifika mbali sana kimichezo,binafsi niipongeze kanda ya mashariki(Pwani na Morogoro) ambayo ilimtoa shujaa Charles Boniface Mkwasa "Master".

Baada ya kumaliza Shule Charles Boniface Mkwasa aliibukia katika timu ya Mseto FC ya Morogoro mwaka 1973 kama beki wa kati na kiungo hodari.

Charles Boniface Mkwasa aliiwezesha Mseto FC kuwa timu ya kwanza Tanzania kutoka nje ya Dar es Salaam kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania mwaka 1975.Mseto FC ndio Mabingwa wa kwanza Tanzania kutoka Morogoro kuchukua ubingwa mdomoni mwa Simba na Yanga kutoka Dar es Salaam.

Mwaka 1976 Charles Boniface Mkwasa akasajiliwa na timu tajiri ya Mkoani Morogoro Tumbaku FC aliyoichezea hadi mwaka 1979 alipong'olewa na dau la Yanga SC, wakati huo Yanga SC ilikuwa imepoteza makali yake kufuatia mgogoro mkubwa wa mwaka 1976 ulioigawa timu hiyo na kuzaliwa Pan Africans.

Baada ya nyota wengi wa Yanga SC kukimbilia Nyota FC klabu nyingine kubwa iliyokuwepo Mkoani Morogoro na wengine walio kwenda kuasisi Pan Africans.

Yanga SC timu kutoka Jangwani,Dar es Salaam ikaanza kujiumba upya kwa kumsajili Charles Boniface Mkwasa kama kiungo bora na nyota wengine.

Mwaka 1979 ndio mwaka ambao Charles Boniface Mkwasa alijiunga na timu yake kipenzi Yanga SC aliyoichezea kwa miaka 10 bila kuhama mpaka anastaafu mpira wa miguu mwaka 1989.Ndiye kiungo mahiri kuwahi kutokea nchini na ndiye kiungo bora wa muda wote wa Yanga SC.

Mkwasa aliweza kuichezea Yanga SC kwa miaka kumi mfululizo mpaka alipostaafu mwaka 1989 . Rekodi inayomfanya kuingia kwenye orodha ya magwiji wa klabu hiyo mahasimu wa kweli wa Simba SC na Uzalendo wa dhati kwa timu ya Yanga SC aliyoichezea kwa miaka kumi bila kuhama licha ya madau mazuri na mikataba minono iliyomtaka kujiunga na Simba SC.

Kitaaluma Charles Boniface Mkwasa ni
Mwalimu wa mpira wa miguu, alianza mafunzo yake ya ukocha hapa nchini mwaka 1988 mwaka mmoja kabla hajastaafu soka . Uwezo mzuri ulimpa fursa kwenda nchini Brazil mwaka 1991 kuchukua diploma ya taaluma ya ufundishaji mpira wa miguu.

Alionesha uwezo mzuri darasani na mafunzo kwa vitendo na aliporudi nchini alirejea kwenye klabu yake kama kocha msaidizi chini ya aliyekuwa Kocha wa Yanga SC hayati Syllersaid Mzirayi.

Mwaka 2000 Charles Boniface Mkwasa alielekea Ujerumani kusomea diploma nyingine ya ukocha na kupata leseni ya daraja A .

Kwa hakika sio wana Morogoro au Yanga SC wanaofurahia matunda ya Mwalimu Mkwasa bali pia Tanzania Prisons mwaka 1999 akiwa Kocha Mkuu aliiwezesha kuibuka mabingwa wa ligi ya Tanzania akiwapiķu vigogo Yanga na Simba kama alivyofanya mwaka 1975 akiwa mchezaji na sasa akifanya hivyo hivyo kama Kocha.

Mwaka 2001 aliitwa kwenye timu ya Taifa akiwa na Syllersaid Mziray chini ya Mshauri wa Ufundi, Mjerumani Burkhad Pape katika kikosi Taifa Stars ambapo Taifa Stars ikatwaa ubingwa wa Kombe la mataifa manne, Castle Cup.

Mwaka 2002, Mwalimu Mkwasa akiwa na Mwalimu Syllersaid Mziray wakaifikisha tena timu ya Bara kwenye fainali ya Kombe la Challenge na kutwaa Ubingwa.

Nikukumbushe tu ndugu msomaji Mwaka 1999 Charles Boniface Mkwasa ndiye alikuwa Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Prisons ya Mbeya, na kuipa ubingwa wa Tanzania.

Kwa mafanikio, Yanga SC wakamchukua kama kocha Mkuu mwaka 2001, akimrithi Raoul Jean Pierre Shungu kutoka DRC.

Mwaka huo 2001 akaifikisha Yanga SC hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika ikatolewa na Mamelodi Sundwons ya Afrika Kusini baada ya kufungwa 3-2 nchini Afrika ya kusini na kutoa sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza mechi ambayo watu walijaa sana Uwanja wa CCM Kirumba,Mwanza.

Mwaka 2006 Charles Boniface Mkwasa akaajiriwa kama Kocha Mkuu wa timu ya Miembeni ya Zanzibar na kuipa ubingwa wa Zanzibar mbele ya timu kali za Malindi,Mlandege na KMKM za Zanzibar na akaenda Mbele zaidi na kuipa timu ya Miembeni FC ubingwa wa Kombe la Mapinduzi mbele ya vigogo wa Bara, Mtibwa Sugar, Simba SC na Yanga SC.

Shujaa Charles Boniface Mkwasa ni mshindi wa mataji ndani na nje ya Uwanja, akiwa anacheza alitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara 1975 na Mseto, 1981, 1983, 1985, 1987 na 1989 na Yanga SC, Ligi ya Muungano 1983 na 1987, wakati pia walikuwa washindi wa pili wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mwaka 1986.

Akiwa kocha, Charles Boniface Mkwasa ametwaa mataji ya Ligi Kuu ya Bara katika miaka ya 1991, 1992, 1993 na 2015 akiwa na Yanga SC,

Ligi ya Muungano 1991 na ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1993 mjini Kampala, Uganda.Mwaka 2006 akiwa na Miembeni FC ya Zanzibar ametwaa Ubingwa wa Zanzibar na Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi,

Ametwaa pia Ngao ya Jamii mara mbili, mwaka 2001 na 2014 akiwa na Yanga SC- na amekuwa Kocha Bora Tanzania mwaka 1999 na 2005 na kwa wiki mbili ndani ya mwezi December 2019 alizokaimu ukocha wa Yanga amekuwa kocha bora wa mwezi December 2019.

-Ushauri wangu kwa timu ya Yanga SC.

Charles Boniface Mkwasa ni zao la Yanga SC na Gwiji ndani ya klabu ya Yanga SC,Makocha wanaohitajika Yanga SC ni vyema wangekuwa wale ambao wanaifahamu vyema klabu ya Yanga na soka la Tanzania kwa ujumla,

Uzoefu wa soka la Afrika sambamba na kuhimili presha ya timu zenye mashabiki wenye mihemko kama Yanga ndiyo inapaswa kuwa sifa ya Kocha wa Yanga SC.

Charles Boniface Mkwasa ndiye aliyekaimu ukocha mkuu wa Yanga baada ya Mwiny Zahera na kwa mwezi mmoja akawa Kocha bora wa mwezi December 2019,Aliwahi pia kuwa Kocha alichukua mikoba Kocha Raoul Shungu mwaka 2001.

Nilitegemea Uongozi wa timu ya Yanga SC ungeamua kubaki naye moja kwa moja kwa kumpa mkataba wa kudumu. Mkwasa ana leseni ya juu ya ukocha kutoka CAF na pia ni mkufunzi wa ndani wa makocha, hivyo anaweza kuwa msaada kwa wasaidizi wake kukua na kupandisha viwango vyao akiwa pia amewahi kuinoa mara kadhaa Taifa Stars.

Faida ya Yanga kama ingempa Mwalimu Mkwasa mkataba wa kudumu ni kwamba, hawatatumia kiasi kikubwa cha fedha kugharamia malipo yake,

Mwalimu Mkwasa ni legend wa Yanga SC ndiye mtu anayeijua Yanga nje ndani kwani mbali na kuichezea na kuinoa, pia hivi karibuni alikuwa katibu mkuu wa klabu hiyo kabla ya kujiuzulu.

Mwalimu Mkwasa ana falsafa ya kujenga muunganiko mzuri na kuimarisha kiwango cha mchezaji mmojamoja.

Binafsi naamini mtu wa kuendelea na Yanga kwa sasa ni Charles Boniface Mkwasa,baada ya kukaimu ukocha kwa mwezi mmoja na kufanikiwa kurejesha morali ya wachezaji katika mechi yake ya kwanza na Ile ya mtani wa Jadi Simba na Yanga zilizotoka sare ya 2-2.

Mkwasa anaujua vizuri mpira wa Bongo kuliko wazungu wanaokuja na kuishia kulalamika kwenye vyombo vya habari eti anabaguliwa !

Mwalimu Mkwasa aliweza kuwarejesha wachezaji katika namba zao kama ilivyokuwa kwa (Ally) Sonso na Mapinduzi (Balama) na wakacheza vizuri katika mechi ya Simba na Yanga.

Mkwasa ni Mwalimu aliyeifanya Yanga kucheza soka la kuvutia zikiwemo pasi fupifupi jambo ambalo hapo nyuma halikuwepo. Soka hilo liliwavutia mashabiki wengi ambao walikuwa wakiridhika hata pale timu yao ilipotoka sare ya 2-2 na Simba SC.

Mwalimu Mkwasa ndiye aliyeiwezesha Yanga SC kutinga kwenye hatua ya makundi na kuiongoza Yanga kwenye mechi tano za makundi ya Ligi ya Mabingwa na kuifikisha hatua ya robo fainali Mwaka 2001.

Charles Boniface Mkwasa ndiye kocha ambaye mara kadhaa ameweza kuirejesha Yanga kucheza staili ya kushambulia muda wote ili kuvuna mabao mengi.

Charles Boniface Mkwasa ndiye Mwanafalsafa wa kucheza kwa kushambulia dakika zote,Shukrani Mwalimu Charles Boniface Mkwasa,Yanga SC na Taifa la Tanzania linatambua Mchango wako katika soka la Tanzania.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Sawa sasa mbona Yanga hawampi Ukocha Mkuu mnaleta Wazungu wakati umetoa sifa nyingi sana au ndio ule usemi kuwa Nabii kwao hakubaliki?
Nabii hakubaliki kwao ila huyu mwamba anastahili heshima zaidi pale Jangwani tofauti na ilivyo sasa
 
1955 Ni zamani sana.amekua huyu jamaa.anatakiwa kustaafu..apongezwe pia kwa namna alivyo-handle stress ya kuachwa na mkewe wa ujanani..Dc mstaafu, huku akifundisha mpira.
 
1955 Ni zamani sana.amekua huyu jamaa.anatakiwa kustaafu..apongezwe pia kwa namna alivyo-handle stress ya kuachwa na mkewe wa ujanani..Dc mstaafu, huku akifundisha mpira.

Alimwacha skaebda wapi, mbona wapo wote hadi sasa. Alimwacha akachukuliwa na nani?
 
Back
Top Bottom