Makerere University yatengeneza gari la umeme

Makoye Matale

JF-Expert Member
May 2, 2011
6,491
2,104
KiiraEV.JPG

(Source: Makerere University - Home)

Hatimaye Makerere University kimefanikiwa kutengeneza gari linalotumia umeme badala ya mafuta yanayopanda bei kila kukicha. Hili ni fundisho kwa UDSM, MIST na DIT. Tunasubiri nao watoe angalau kazi nzuri kama hii badala ya kubaki na makaratasi ya kazi za watu katika machapisho. Maprofesa waoneshe ujuzi kwa vitendo siyo kukimbilia posho bungeni.
 
ndg naona umekimbilia lawama kwa vyuo kama kawaida ya jf. hivi vitu mbona vimetengenezwa sana hata veta, juzi kijana wa Ruvuma kaunga unga gari. Issue siyo kutengeneza, issue ni efficiency, reliability na kuweza ku-commercialize hilo gari likaleta pesa. Hata nchi kubwa hawajaweza kuwa na gari la umeme ambalo ni reliable, viko vya kuzungukia mjini with limited capacity.
 
Tatizo siyo Maprofessa , tatizo ni mfumo mbovu wa elimu unaomjenga mtu kuwa mtumwa wa ajira badala ya Ubunifu!
 
Tatizo siyo Maprofessa , tatizo ni mfumo mbovu wa elimu unaomjenga mtu kuwa mtumwa wa ajira badala ya Ubunifu!
Kwani hao wa Makerere wanasoma sayari gani? Kuwa na 'innovative ideas' hakutegemei sana ukubwa au ubora wa elimu tu. Ni lazima uwe na akili ya kuona na kuhoji chanzo cha matatizo yanayoikabili jamii yako na kubuni ufumbuzi wake. Hata hao wa Makerere siyo kwamba hiyo gari iko sokoni inauzwa. La. Ni mradi wa majaribio ambao unaendelea kuboreshwa mpaka pale litakapoonekana linakidhi vigezo kama alivyohainisha MJIMPYA hapo juu.
 
ni mazuri haya magari ila hua yana kuaga na disadvantage ya short distance coverage na weight inayo bebwa na gari inakuaga ni ndogo coz weight kubwa inachukuliwaga na heavy batteries ambazo zinabebwa nyuma..!
 
Hiyo nishati ya umeme inatokana na nini, hydro, diesel, steam au kitu gani? Tusije tukarudi pale pale. Hata hivyo tuwe na mazoea ya kutembelea mabanda ya vyuo vyetu vya nchini wakati wa maonyesho mbalimbali, mwaka huu DIT waliweka gari linalotumia gesi. Kama alivyosema Mjimpya, labda tulinganishe efficiency !
 
Wenzetu wameweza na wanasonga mbele je sisi waTZ tumejifunza nini?
 
Hiyo nishati ya umeme inatokana na nini, hydro, diesel, steam au kitu gani? Tusije tukarudi pale pale. Hata hivyo tuwe na mazoea ya kutembelea mabanda ya vyuo vyetu vya nchini wakati wa maonyesho mbalimbali, mwaka huu DIT waliweka gari linalotumia gesi. Kama alivyosema Mjimpya, labda tulinganishe efficiency !
Hata VETA nao sabasaba walikuwa na gari linalotumia umeme, hivyo tusianze kulaumiana wakati hatuko informed.
 
Kwani hao wa Makerere wanasoma sayari gani? Kuwa na 'innovative ideas' hakutegemei sana ukubwa au ubora wa elimu tu. Ni lazima uwe na akili ya kuona na kuhoji chanzo cha matatizo yanayoikabili jamii yako na kubuni ufumbuzi wake. Hata hao wa Makerere siyo kwamba hiyo gari iko sokoni inauzwa. La. Ni mradi wa majaribio ambao unaendelea kuboreshwa mpaka pale litakapoonekana linakidhi vigezo kama alivyohainisha MJIMPYA hapo juu.

Tembelea VETA wanalo kitambo gari la namna hiyo
 
Safi sana, wamejaribu , wameweza & wanasonga mbele kwa vitendo.
Sio sie tunakalia taarabu tu & kuvuana magamba daily tantalila nyingiiiiiii
Shame!

Il Gambino.
 
Back
Top Bottom