Makapuku Forum

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba amewaonya Watu wanaomsema vibaya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dk.John Magufuli, ametoa kauli hiyo Bungeni huku akikumbusha kuwa huo siyo utamaduni wa Watanzania———“mwacheni apumzike"
20210413_123406.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhandisi Mtemi Msafiri amethibitisha kutokea kwa vifo vya Watu watatu kufuatia kubomoka kwa Daraja linalounganisha Barabara Kuu ya Mwanza Sirari lililopo Mtaa wa Mwangaza Mjini Tarime, kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mara.

Amesema Watu hao walikutwa wakiwa wamefariki baada ya Daraja kubomoka na inaaminika walikuwa wanakatiza Juu ya Daraja wakati linabomoka au huenda walitumbukia baada ya Daraja kubomoka, uchunguzi zaidi unaendelea.

Kwa upande wake Meneja Wakala wa Barabara mkoani Mara, Mhandisi Mlima Ngaile amesema kuwa tayari Serikali inahamisha fedha haraka kwa ajili ya kutengeneza Daraja hilo lililobomolewa na mvua ili kurudisha mawasiliano ya pande mbili.

"Barabara hii ya Sirari Mwanza ilikuwa imetengewa bajeti tayari sasa tutasitisha kazi nyinngine ili kuleta fedha kwa ajili ya matengenezo ya haraka, Mkandarasi anakuja ili aweke kambi hapa amalize kwa wakati”———Ngaile
20210413_123620.jpg
20210413_123756.jpg
20210413_123817.jpg
20210413_123842.jpg
20210413_123901.jpg
 
“Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tunafuatilia malalamiko ya wadau wa Tasnia ya Habari juu ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Ndugu Lusabilo Mwakabibi, kuweka chini ya ulinzi Wanahabari, tunaomba Wanahabari wawe na subira wakati allegations hizi za kusikitisha zinafanyiwa kazi”———Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
20210413_124115.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom