Tuweke kwanza pembeni "upuuzi wa lee"
Kwa wapenzi wa kabumbu baada ya kumalizana dodoma macho na masikio na dunia itasimama kwa mda kushuhudia mtanange kabambe wa vigogo hawa ...bwanabwaaanaaah usikubali kusimuliwa .
Anyway baada ya futuhi kujihakikishia usajili wa mwaka mzima watawashuhudia wenzao arseno wakijaribu kuona kama watamshinda huyu le geneous Antonio na falsafa zake alizowamezesha watukutu wa bilionea yule bwana ...
Twende sawa ....

ARSEN WENGER ni Kocha mwenye uwezo Mkubwa sana wa kuzibadili big match zikawa mechi za kawaida kabisa ...... Na hichi wana Arsenal wanakifahamu sana japo wanajificha. Baada ya kushtuka na kujifunika shuka kushapambazuka mzee huyu alikumbuka kipigo alichompa chelsea na kupelekea mzee Antonio achange mawwzo ..tumeona namna mapinduzi ya mfumo wa 3:4:3 yalivyomfaidisha babu Wenger katika michezo ya mwishoni mwa Msimu. Majeruhi alionao Bado wanampa wakati mgumu sana kupigana vita hii.
Apooo chachaaaaaa....

ANTHONY CONTE teyari gari lake lilishawaka mda sana, ile score timing na winning time aliyokuwanayo ndio kitu kilichoifanya Chelsea iwe katika ubora wao Msimu huu..... Amekuwa mgumu sana na bora zaidi katika vitu hivyo viwili.... Muda wa kufunga na namna ya kumaliza mchezo. 3:4:3 hii ndio imekuwa sumu yao na maziwa yake mwenyewe.

Kukosekana kwa Koscielny mtu ambaye amekuwa mhimili wa Arsenal katika back line Bado kutapunguza ubora na uimara wa Arsenal katika mchezo huu....... Ni ngumu kukaa Siti ya mbele huku beki wako watatu ni Nacho, Bellarin na Holding. Njia pekee ya usalama wa Peter Cech ni coquelin na Xhaka eneo la kiungo.
Kumchezesha Alexis Sanchez kama mshambuliaji wa mwisho mbele, kunaweza kupunguza mashambulizi kwa kiasi kikubwa sana. Hii inatokana na ubora wa Alexis Sanchez akiwa anakimbia na mipira kuliko kukaa kusubiri mipira ije katika eneo lake.
Hii ni FA na mara nyingi babu Wenger akiwa akijua sana namna ya kushinda michezo hii ila shaka yangu ni namna wanavyojipanga katika eneo la beki na mfumo atakao ingia nao....... Hii ni vita nyingi kwa Arsen Wenger na arsenal kama chochote kitatokea.
Tujutane baadae kuedit matokeo
Arsenal _vs Chelsea_