Makapuku Forum

Watu walio fanya kaz miaka mingi

_95908442_philip2afp.jpeg
_93039574_2ae0c521-9ac5-48b8-bf62-64355c050ec1.jpeg

1.David Goodall, Mwansayansi mkongweAustralia

Mkongwe huyo wa miaka 103 mwaka jana alishinda kesi kuendelea kufanya kazi katika chuo kikuu kilichoko magharibi mwa Australia cha Edith Cowan huko Perth.

Dr Goodall aliagizwa kufanya kazi akiwa nyumbani 2017 huku kukiwa na wasiwasi kuhusu usalama wake, lakini chuo hicho baadaye kilisema, nafasi nzuri imepatikana katika tawi la chuo hicho lililoko karibu na makaazi ya mwanasayansi huyo.

Dr Goodall amechapisha matokeo ya utafiti zaidi ya 100

Dr Goodall, aliyelazimika kuachana na uigizaji, kutokana na kutoweza kuendesha gari kwenda kufanya mazoezi kwasbabau ya matatizo ya kuona, amesema ameshukuru kuwa chuo kikuu hicho kimeweza kumpa nafasi.
Dr Goodall, ambaye sasa anashikilia wadhifa wa mtafiti muandamizi katika chuo hicho, amechapisha zaidi ya nyaraka 100 za utafiti katika ekolojia katika kipindi cha miaka 70.
 
2.Anthony Mancinelli, Kinyozi mkongwe duniani

Mkongwe huyu wa miaka 106 kutoka kaunti ya Orange jimboni New York ametuzwa rasmi sifa hiyo na Guinness Book of World Records mnamo 2012.

Lakini Mancinelli, ambaye amekuwa akinyoa nywele kwa zaidi ya miongo 9 anaendelea kufanya kazi.

"Usisite. Ukistaafu na umezeeka katika unachokifanya - tafuta kingine cha kufanya. Usistaafu," alisema katika mahojiano hivi karibuni na WCBS 880.

Anakumbuka kwa furaha siku za kwanza alipoanza kufanya kazi dukani ambapo vinyozi walilazimika kutoa huduma nyingine za kuondosha maumivu na hata kutumia ruba kupunguza shinikizo la damu.

_95909958_capture.png
 
3. Mastanamma Nyota wa India

Ana miaka 106 na huwavutia watu wengi kwenye kipindi chake cha upishi India.

Anatumia mbinu rahisi za upishi anazoziita "mbinu za kijijini". Hupika chakula kitamu cha kitamaduni India

Mastanamma, anatoka jimbo la India kusini Andhra Pradesh, na anasema upishi sio mgumu na mtu yoyote anaweza kupika.

Fikra ya kuanzisha kipindi chake ilitokea kwa kitukuu chake aliyechapisha video zake akipika.

_95909959_capture1.png
 
4.Shigeaki Hinohara - Huenda daktari mkongwe zaidi anayefanya kazi kutoka Japan

Mkongwe huyu wa miaka 105 wenzake humtambua kama mali ya kitaifa inayoishi Japan

Dr Hinohara anaongoza taasisi tano kando na kuwa rais wa hospitali ya kimataifa ya St. Luke's Tokyo

Na bado huitembelea hospitali hiyo kila siku kuwakagua wagonjwa.

Babake, ni kiongozi wa dini ya kikristu inaarifiwa alimpa ushauri muhimu:
"kuwa na malengo makubwa na uyatimize maishani kwa hikima. Huenda usiyatimize ukiwa hai, lakini usisahau kujaribu, ndipo utaweza kufanikiwa."

Dr Hinohara amechapisha maelfu ya nyaraka ya kitabibu, na ameandika mamia ya vitabu.

_95909292_capture2.png
 
View attachment 514341
Ngumu kuamini aiseeeee

Sis miaka 45 mgongo ushakata sentaboritiiii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom