Makapuku Forum

Makapuku Forum

6fc762a1fccf4bd5a8b256677ef0d948.jpg
 
ZABURI 91

5.Hutaogopa hofu ya usiku,wala mshale urukao mchana.

TUOMBE

Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi,asante sana kwa ulinzi mchana kutwa,tunaomba toba kwa yote tuliyokosea kwa mawazo maneno na matendo,uturehemu twakusihi.
tunajikabidhi mikononi mwko usiku wa leo tueushe na hatari na ajali mbalimbali tusigope hofu za usiku maana upo pamoja nasi usiku wa leo unatukumbatia,asante kwa kuwa utatupa kushinda
Nakuomba uwaponye wagonjwa wote majumbani na hospitali zote nyoosha mkono wako kwa mpendwa wetu Bitoz BABA damu ya Yesu inene mema,apate uponyaji wa haraka na asipungukiwe.
Angalia wajane,yatima wape faraja kuu.
Malaika walinzi wazunguke vitanda vyetu kutulinda
Wabariki wasafiri wafike salama.
Asante Baba kwakuwa utatenda sawa na mapenzi yako ,tunaomba na kushukuru Amen
USIKU MWEMA
MBARIKIWE
hatuogopi hofu ya usiku wala mshale urukao mchana, amen
gud nite mom
 
Oooh Yeah Obe asante sana"... my coat of many colours that my mother made it for me...." nakumbuka akiimba na Porter Wagoner...Ooooh gitaaa gitaa..ubarikiwe sana


Just Someone I used to Know..... binafsi naupenda 'Holding On To Nothing' na 'Dad was an old time preacher man'.

Siku moja nitakuja na gitaa la Porter Wagoner

Halafu ujue wewe ni uzao wangu kabisa, sema wewe tu hujajua😉 ( Shunie usibadili maneno hapa shangazi yangu wewe)

 
Just Someone I used to Know..... binafsi naupenda 'Holding On To Nothing' na 'Dad was an old time preacher man'.

Siku moja nitakuja na gitaa la Porter Wagoner

Halafu ujue wewe ni uzao wangu kabisa, sema wewe tu hujajua😉 ( Shunie usibadili maneno hapa shangazi yangu wewe)


Asante Obe nimefurahi kusikiliza hawa wakongwe sijawahi kuchoka kuwasikiliza
 
ZABURI 108

1.Ee MUNGU ,Moyo wangu u thabiti,Nitaimba ,nitaimba,nitaimba Zaburi,Naam kwa utukufu wangu

2.Amka ,kinanda na kinubi Nitaamka alfajiri.

3.Ee BWANA nitakushukuru kati ya watu,Nitakuimbia Zaburi kati ya mataifa

4.Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,Na uaminifu wako hata mawinguni.

5.Ee MUNGU utukuzwe juu ya mbingu Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.

TUOMBE

Tunakushukuru Baba wa Mbinguni kwa kutuamsha salama,wako wengi walitamani kuiona siku ya leo hawakuweza tunakurudishia sifa na shukurani Mfalme wa Amani.
Nakushukuru kwa kukuimbia kati ya mataifa maana fadhili zako ni kubwa
Ponya wagonjwa wote BABA ,Watie moyo waliovunjika moyo na wale wote wanaopitia changamoto mbalimbali kwa namna ya pekee tunamkabidhi kwako na tunamuombea mpendwa wetu BITOZ,mtie nguvu ,takasa dawa anazotumia takasa mahali anapolala,takasa madaktari na wote wanaomhudumia,Baba tunaomba uponyaji wake uwe wa haraka .
Tunawakabidhi yatima ,wajane,wahitaji baba watetee,wasipungukiwe.
Imarisha imani zetu ili tuweze kukitegemea wewe tu
Walinde wasafiri wote wafike salama ,nchi kavu,majini,angani
Tuma malaika wako wa yltuzunguke watuongoze tufanye kazi kwa bidii na kukupenda wewe tu
bariki kazi za mikono yetu,asante
Naikabidhi jumanne ya leo iwe ya kipekee, tembea pamoja nasi baba.
Tunaomba na kushukuru
Amen

NAWATAKIA SIKU NJEMA MUNGU AWABARIKI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom