Makapuku Forum

Tunashukuru aisee
 
aisee
asante Bitoz kwa top 10
 
Kama kweli nitumie picha ya hapo mpaka kuna kibao kimeandikwa sasa unaingia mkoa wa pwani
Pale penye kibao hicho ni pale darajani panaitwa mpakani,hapo ndipo alipofia marehemu aliyekua mwenyekiti wa FAT WA MKOA MBEYA MIAKA YA NYUMA SASA HV TFF...KWA AJALI YA GARI BUS SCANDNAVIA ENZI HIZO,SIKUMBUKI MWAKA..RIP
 
sawa mkuu
 
Muziki: Maneno yakishindwa Weka Muziki

Habari za kutwa nzima ya leo Makapuku wenzangu. naamini kabisa tumekuwa na wakati mzuri jumatatu hii na sasa tunaenda kuikamilisha ili siku nyingine ianze. Ndiyo maisha, tunabadili tarehe tu na siku za juma zinabaki zilezile.

Nimekuwa na wakati mzuri leo, nashuku. Asante kwa wadau wote mnaopendezesha Jukwaa hili, wote kwa ujumla kwa michango tofauti tofauti, kuanzia wakati wa magazeti, sala, historia, UF, na chats za hapa na pale ilmradi tu kila mmoja anabaki kuwa na amani na forum hii.

Pole Bitoz kwa maumivu na ni habari njema kusikia unaendelea vizuri, hii ni kwa makapuku wote wanaougua na kuuguliwa.

lakini pia hongera kwa makapuku wote waliopata mishahara leo, waliokopa wakakopeshwa leo. Ni jambo zuri.
Sasa turudi kwenye ka-kipengele ka Muziki na hasa tukiangalia gitaa nami bila hiyana nakuletea kitu ambacho nachagua nikiamini kabisa utakipenda ukijipa muda wa kukisikiliza.

Leo tunaangalia 'country music'. Oh yeah, sauti nzito na gitaa la bass ndiyo tumeyazoea. Sitoangalia sauti nzito leo. Nitakusikilizisha sauti nzuri, tamu, mchanganyiko wa limau na sukari. Ndiyo, naamini unamjua ninayemleta kwako usiku huu, Dolly Parton.

Niandike nini ambacho hujawahi kukisikia kuhusu mwanadada huyu ambaye ni mmoja wa watu waliobahatika kuwa na uwezo wa kuimba na kupiga vyombo vingi vya muziki, gitaa likiwemo.

Ni mwanamke ambaye katika tasnia ya muziki anaweza kuwa katwaa tuzo nyingi sana kuzidi wanamuziki wengi maarufu unaowafahamu. Nyimbo zake zaidi ya 25 zilishika namba 1 katika chati za Billboard huko USA.

Hii ni mbali ya tuzo 9 za Grammy, 10 za Country na katajwa katika Academy mara mbili.

Kawa walivyo waimbaji wa country walio wengi, Dolly anajua kupiga gitaa. Nyimbo zake maarufu ni kama Jolene, The Coat of many colors, Pain of Loving You (ninaupenda huu). Love is like a butterfly.

Mtizame clip hii ya YouTube akicharaza gitaa kwa umahiri

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…