Watu mna misemo ninyi...ngoja tuuingize kwenye hansadi kamili za Bunge la Makapuku ili urasimishwe kisheria...ila hujaweka wazi huyu mume masikini ni mume wa Dar ama mume wa kijijini!
Leo ni siku ya kupeana mrejesho wa tulichoingiza ama kupoteza kwa week inayomalizika ya kazi...marehemu bibi wa mjomba wa rafiki yangu aliwahi niusia kwamba "ili ujue unapoelekea ni lazima uwe na dira ya kukuongoza". Ndiyo maana mimi na mama yenu ikifika siku hii ya leo kwanza tunaenda kumshukuru aliye juu kisha tunarudi nyumbani ku review ni wapi tulipo na ni kwanini hatukufikia malengo ya week! Kwa hiyo mkuu leo nipo tu Ipuli kijijini huku!
Ukiwa mwanaume wa Dar na unaona wingu kwenye maisha dawa ni kutafuta mwanamke mwenye reception nzuri kisha wewe kuwa mtiifu kwa bosi wake ili ampe mkeo safari nyingi za 'kikazi' kumwongezea kipato cha kujiunga vikundi vingi vya vikoba!