Makapuku Forum

Elimu ni nini? Kwa nini huyo mwenye ng'ombe moja kwa moja anachukuliwa kuwa hajaelimika? Hapa ndipo mzungu huwa namvulia kofia. Alipofika na kutukuta sehemu nyingi hatuna mashule basi akatubatiza kuwa tulikuwa wajinga tunaoishi gizani nasi tukamuamini. Wakati huo huo unakuta mzee anajua mimea zaidi ya 2,000 na matumizi yake kitiba tena bila daftari. Huyu kweli naye hajaelimika? Na kuanzia hapo Waafrika ikawa down hill kuelekea kwenye utumwa wa kisaikolojia!
 
Katika zoezi la kupiga picha za vitambulisho vya shule, mpiga picha alimwambia mwalimu mkuu kwamba picha moja ni 500 kwa kila mwanafunzi.. Mwalim mkuu akawaambia walimu wa darasa kuwa wawaambie wanafunzi walete 1000 kila mmoja wao kwa ajili ya picha.. walimu wa madarasa wakawatangazia wanafunzi kuwa kila mmoja alete 1500 kwa ajili ya picha.. watoto wakasema kwa mama zao wao kuwa kuna kupiga picha na gharama ni 2000. Mama sasa kwa baba wa familia.. " Baby hizi shule za siku hizi kwa kupenda pesa.. kuna mchango wa picha 5000 mpenzi wangu mtolee mwanao apate kitambulisho.."

Asa namna hii wizi utaisha Tanzania ?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…