Ni kweli. Kwa hali ya Tanzania ilivyo hatupaswi kuwa na njaa. Nimepitia California huku wana ukame wa miaka 10+ lakini huwezi kujua na hata bila msaada wa majimbo mengine wanaweza hata kujilisha wenyewe. Wakulima wakubwa 50 hivi wanaweza kulisha jimbo mamilioni ya watu na kila kitu ni irrigation. Wamechimba visima virefu na kujenga mabwawa makubwa makubwa. Sasa mvua zinanyesha na maji haya yanavunwa na kuhifadhiwa.
Kama nilivyosema hapo juu, sisi priorities zetu ziko misplaced na kilimo bado hakijapewa nafasi inayostahili. Tungekazania mapinduzi ya kilimo tungeingia hata kwenye viwanda vyepesi tukiwa na watu walioshiba. Lakini mkazo wetu ni madege na kujengewa viwanda vikubwa vikubwa Wachina. Huwezi kuwa taifa la viwanda wakati watu wako wana njaa!