Makapuku Forum

1990 - Waziri Mkuu wa Uingereza, Margaret Thatcher anajiondoa kwenye uongozi wa chama chake cha Conservative hali inayopelekea kutochaguliwa kuwa Waziri Mkuu tena wa Nchi hiyo.

Bibi Thatcher alisifika kwa uongozi wake shupavu na hodari hali iliyomfanya kupachikwa jina la Iron Lady.
 
1982 - Yakubu Aiyegbeni anazaliwa.

Ni straika wa zamani Portsmouth, Middlesbrough, Everton na timu ya taifa ya Nigeria.

Alikosa goli la wazi kwenye kombe la dunia mwaka 2010 akiwa yeye na goli tu.
 
1985 - Asamoah Gyan anazaliwa.

Ni straika wa zamani wa Sunderland ambaye kwasasa anakipiga Uarabuni.

Anakumbukwa kwa kukosa penati ambayo kama angeshinda Ghana ingekuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kuingia katika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…