Makapuku Forum

Makapuku Forum

1.Yesu;
Yesu alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita

Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kuanzia ujio wake
Mbali ya hayo, zaidi ya nusu ya wanadamu wote wanamuamini kuwa Mwana wa Mungu (wanaoitwa Wakristo) au walau nabii (hasa Waislamu)
Yesu hakuacha maandiko yoyote. Habari zake zinapatikana hasa katika Biblia, kwa namna ya pekee katika Injili.

Nje ya Ukristo kuna habari fupi kuhusu Yesu katika maandiko ya waandishi Waroma, Wagiriki na Wayahudi. Habari hizo zinaangaliwa sana kwa sababu zimetungwa na watu wasiomwamini Yesu. Kwa ujumla zinathibitisha ya kwamba Yesu alikuwepo, alikuwa na wafuasi huko Roma na ya kwamba awali Waroma hawakuelewa tofauti kati ya wafuasi wake na Wayahudi.

Nchi ambayo Yesu alizaliwa akafundisha ni nchi ileile ambayo Mungu aliwaahidia Waisraeli tangu zamani za Abrahamu, ni nchi ileile waliyoiteka chini ya Yoshua, ni nchi ileile waliyoirudia kutoka utumwani Babeli.
Waumini wake wanaunda Kanisa la Kikristo ambalo linapatikana leo katika madhehebu mengi. Karibu wote wanamwamini kuwa Mungu aliyechukua umbile la mwanadamu au, kwa lugha nyingine, kuwa Mwana wa Mungu.

Wakristo wengine wanaamini kuwa yeye ni mtume wa pekee wa Mungu ila si Mungu.
Katika dini ya Uislamu, Yesu anajulikana kama Nabii Isa. Waislamu wanaamini kuwa yeye alikuwa ni nabii wa Mungu ila hakuwa mwana wa Mungu wala Mungu.
Maisha yake yamekuwa msingi wa sikukuu mbalimbali zinazosheherekewa katika nchi nyingi duniani, kama vile Noeli au Krismasi (kuzaliwa kwake), Epifania (kuonekana kwake na kubatizwa kwake), Majilio (kuandaliwa kwa ujio wake wa kwanza na kutarajia ujio wa pili), Kwaresima (mafungo na mateso yake), Ijumaa Kuu (kifo chake); muhimu kuliko zote ni Pasaka (kufufuka kwake).

images

****niliishiwa MB jana****
 
Back
Top Bottom