Camilo Cienfuegos
JF-Expert Member
- Apr 23, 2015
- 19,234
- 68,268
Leo katika Historia:
1936 - Jesse Owens ashinda mbio za mita 100 na kushangaza watu wengi akiwemo kiongozi wa Ujerumani Adolf Hitler katika mashindano ya Olimpiki ya majira kiangazi huko Jijini Berlin.
Leo katika Historia:
1960 - Niger yajipatia Uhuru wake toka kwa Ufaransa.
Leo katika Historia:
1975 - Inatokea ajali ya ndege huko Agadir, Morocco na kuua watu 188 baada ya ndege kubwa ya Boeing 707 kudondoka.
Inaelekea simu yako kiboko
Leo katika Historia:
2004 - Mnara wa Liberty huko Marekani " Liberty Statue " wafunguliwa upya mara baada ya kufungwa kwa muda baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi ya September 11, 2001 huko Marekani.
Leo katika Historia:
2005 - Mahamodou Ahmadnejad achaguliwa kuwa Rais wa Iran.
Moja kati ya Marais waliokuwa na msimamo dhidi ya Nchi za Magharibi.
Leo katika Historia:
2014 - Kunatokea tetemeko la ardhi huko Yunnan nchini China na kuua takribani watu 617 na kujeruhi 2400.
Leo katika Historia:
1934 - Jonas Savimbi anazaliwa.
Alikuwa ni kiongozi wa kikundi cha Waasi kilichojulikana kama UNITA ambacho kilikuwa kinapambana dhidi ya Serikali ya nchi ya Angola.
Savimbi alifariki dunia mwaka 2002.
Leo katika Historia:
1950 - Ernesto Samper anazaliwa.
Alikuwa ni Rais wa 29 wa Colombia.
Alisifika kwa kutumia vibaya mali ya umma na kujitajirisha sana.