Makapuku Forum

Leo katika Historia:

1966 - England yashinda kombe la Dunia baada ya kumfunga Ujerumani mabao 4-2 baada ya Extra time.

Michuano hiyo ilifanyika Kwao England, Na huo ndio ubingwa pekee waliofanikiwa kutwaa mpaka leo.

Leo wanatimiza miaka 50 baada ya kutwaa ubingwa huo. Baadhi ya mastaa waliocheza fainali hiyo ni pamoja na Sir Bobby Chalrton, Nahodha Bob Moore, Mfungaji wa mabao matatu ya England siku ya fainali, Sir Goeff Hurst.
 
Leo katika Historia:

1974 - Vuguvugu la Skendo ya Watergate inamfanya Rais wa Marekani Richard Nixon kuwasilisha nyaraka muhimu za ikulu ya Marekani kama alivyoagizwa na Mahakama nchini humo.

Skendo ya Watergate ilikuwa ni mbinu chafu zilizokuwa zinafanywa na Utawala wa Rais Richard Nixon dhidi ya Wapinzani wake.

Skendo ilikuja kumfanya ajiuzulu Urais. Na kuwa Rais wa kwanza na pekee wa Marekani Kujiuzulu wadhifa huo.

Tuatakuja kuona mbeleni katika Historia.
 

Hawachukui tena
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
.................
 
Hahahahahahahahahahaha hii habari umenichekesha sana
Kumbe walitwaa miaka 50 iliyopita?? Pole sana kwa mashabiki wote wa England
 
Leo katika Historia:

1975 - Jimmy Hoffa aliyekuwa Kiongozi wa Wafanyakazi, anatoweka katika Parking ya mgahawa wa Machus Red Fox huko Michigan nchini Marekani na hajawahi kuonekana tena mpaka leo.

Licha ya kuwa ni kiongozi wa Wafanyakazi pia alikuwa ni Mwanaharakati hali iliyopelekea kutifautiana na Watawala.

Ilipofika July 30 mwaka 1980 ndugu zake walitangaza kuamini kuwa Jimmy atakuwa amefariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…