Makapuku Forum

7. Bagh-e Fin, Kashan, Iran hapa ndipo ilipo ile bafu ya Kashan Fin, ambayo Amir Kabir, kansela wa Qajarid, aliuwa na watu(assasins) walo tumwa na mfalme Nasereddin Shah in 185 (kama hukusoma historia pole)

Haijulikani ilianza kujengwa lini lakini kwa kuwa ilimalizw kutengenezwa mnamo mwaka 1590 hii ndo Garden kongwee penginepo kuliko zoote kati ya hizi kumi bora hii imejengwa ki dizain ya “chahar bagh” kama ilivo andikwa kwenye Qur'an kuwa huko peponi kuna mito miwili ina pishana aka ina cross na waliijenga hivo kwa kuvuta na bomba maji yanayo tiririka milimani , kwa wale wasoma maandiko wenzangu mtakuwa mme nielewa najua
 
Huu uzi unazidi kunawiri
 
 
Number 6, Desert Botanical Gardens, Phoenix, Arizona walio ianzisha ni Arizona Cactus na Native Flora Society mwaka1937, bustani ina maua zaid ya aina 21,000 , zaid ya taxa 4000.

Kwa wale tulo fika Arizona tunajua kuwa ni jua kali sana na kuna hali ya ujangwa so ukiiona hyo bustan nadhan uta enjoy
 
 
Number 4, Gardens at the Versailles Palace, France haya maelezo na tia kiingereza kama yalvo ekwa vile vilee "The gardens are now one of the most visited public sites in France, receiving more than six million visitors a year." Bustan hizi zina chukua hekta zaid ya 800 ilijengwa na Louis XIV’s ambaye alisema jumba la kifalme lazma liwe na bustan nzuri pia ajiita yeye ni mfalme wa jua hivo alihitaji kivuli
 
Iko poa sana hii
 
Number 3, Majorelle Garden, Marrakech, Morocco miaka ya 1920 wakati mchoraji mmoja kutoja ufaransa alipo chora bustani ya kufikirika tuu na kuiweka kwejye maonyesho huko Paris hakujua kama inaweza kuwa kweli na mchoraji huyo si mwingine bali ni
Majorelle, hii ni bustani nzuri kweli kweli, na pembeni yake kuna majengo ya maonesho ya sanaa mbali mbali na pia maktaba ya vitabu vya mafundisho mbali mbali ya ki Islam

Kwa maoni yangu hii ndo ilifaa kuwa ya kwanza lakini ndo bas tena nawa achia wenyewe
 
 
Number 2, Claude Monet’s Garden at Giverny, France kwa miaka 43 mchoraji Oscar-Claude Monet, aliishi nyumbani kwake kijijini huko Givenry akijaribu kutengeneza bustani inayo fanana na michoro yake ya bustani, na ilimchukua miaka hiyo kufanya bustan hiyo ionekane hivo ilivo , miezi mizuri ya kutembelea hapo ni mwezi wa 4 hadi wa 10, ni bustani nzuri kweli kweli nilikuwa hapo mwaka 2009, kwa kweli nilipata mawazo ya kuzamia Ufaransa
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…