Makapuku Forum

Sasa siku zote huwa tuna panga gharama za harusi na kamati na ishu kama hizo
Lakini pia tuna waombea maharusi waishi pengine milele kabisa
Lakin pia watu hao wanapo gombana na kuachana officially inakuwepo kitu inaitwa talaka

Talaka nayo ina gharama zake na hutegemea na wanaopeana talaka wenyewe
 
So leo nna tuna cheki
Talaka ambazo zimekuwa za gharama kubwa kuliko zotee, na zina husisha pesa ambayo aliyekuwa mke alipewa

Yaan the most expensive divorce settlements in the world.

Pesa hizi ni za kimarekani so dola moja ni sawa na shillingi za ki tz 2000 na zaid

Mta kalukuleti hapo
Karibu
 
Waiting......
Uwe unachaji simu mapema lol..
 
Number 10, Michael na Maya Polsky – USD 184 million
Michael Polsky was the owner

michael alikuwa ana kampuni ya kuuza umeme ya skygen huko Illinois na baadaye akaiuza kwa usd 450 milioni, na mnamo mwaka 2003 Maya alidai talaka na aka sema ana hitaji wapigane pasu kwa pasu kupitia mwana sheria wake, kwani alidai alipo olewa na Michael bado muoaji alikuwa ni masikini na ametajirika wakiwa ndani ya ndoa

Jaji alikubali na bibie Maya akala kutita ambacho anaendelea kutumbua hata hivi leo
 
Interesting....
 
Rahaaa
 
Number 9, Charles Edgar Fipke na Marlene Fipke – USD 200 million
mnamo mwaka 1991 bwana charls edga alioa, akiwa ni mmiliki wa mgodi wa almas huko Colombia, baadaye alinunua baadhi ya migodi mingine huko Canada, lakin mkewe Charles, bibi Marlene alidai talaka kwakuwa mumewe alishinda sana migodini kuliko nyumbani kwake

Jaji aliamuru Merlin apewe ma millioni hayo, lakini ilibidi bwana charls ashuke kidogo kutoka kuwa mmiliki mpaka kuwa mmiliki wa hisa kwa asilimia 29 tuu
 
Number 8, Arnold Schwarzenegger na Maria Shriver – USD 250-375 million
sasa Arnold si kila mtu ana mjua ee, ile mikanda yeke ile anorld na jane sjui, the terminator hataree
Pia alikuwa gavana wa California
Huyu alikuwa ana piga kimya kimya na mfanya kazi wake wa ndani wa muda mrefu bibi Mildred Baena, mara ya kwanza hakuhisi kama ni mimba yake na alimkataa mtoto
Lakini kama tunavojua Mungu si Jambilo, mtoto alivo fikisha miaka mitatu alifanana sana na mzee ikabidi akubali mchezo
Kilicho fuata ndo hikooo
 
Mungu siyo.........
Mbona mkorofi ww
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
.......
 
Number 7, Roman na Irina Abramovich – USD 300 million
huyu ni kati ya watu matajiri 50 duniani ana utajiri wenye thamani ya USD14.6 billion, na ndiye mmiliki wa timu iliyo nusurika kushuka daraja msimu ulo pita huko England yaan Chelsea na ana visima vya mafuta huko urusi
Baada ya kuchepuka na Daria Zhukova, ambaye ni binti wa mwanasiasa mmoja huko Urusi, aliamua kumpa talaka mkewe na ili bidi amfidie na bibie irina kwa vijpesa vya kujisitiri hvo na waligawana pia baadhi ya vitu walivo miliki kwa pamoja
 
Pale faulo ilipomtajirisha beki 3
 
Number 6, Robert na Sheila Johnson – USD 400 million
walikuwa ndiyo waanzililishi wa BET ila ugomvi wao ukawa ni jinsi BET inavo wafundisha vijana wa kimarekani, Bibie Sheila hakupendezwa na vipindi hivo, kama utani utani hviii, baadaye ndiyo ikatokea talaka
Baada ya talaka hiyo baadate bwana Robert aliiuza BET kwa USD 4 billion, na hadi sasa uwa anakuka bata tuu ni mmoja ya watu matajiri huko Amerika
Naskia huwa ana kuja hata Zanzibar
 
Number 5, Mel na Robyn Gibson – USD 425 million
hii ndiyo talaka yenye gharama kubwa huko Hollywood, baada tu ya mel kukubali kwamba ana mtoto na muimbaji wa ki rusi aitwaye Oksana Grigorieva. Mkewe hakusita kufuta ndoa yao ya miaka 28, kwa kuwa hawakukubakina mahakamani, ilibidi wagawane mali nusu kwa nusu, na walipo enda kumalizia kesi mahakamini
Mel aliamuliwa kutoa nusu kwa nusu mpaka kwenye movie ambazo alikuwa haja zitoa lakini ali rekod akuwa kwenye ndoa, na dola zaid ya 750,000 kila mwaka kwaajili ya malezi ya mtoto
 
Number 4, Craig na Wendy McCaw – USD 460 million
jamaa alikuwa ana miliki kampuni ya simu, basi ilitokea tuu wame chokana kila mtu akachukua chake aka kiamsha
Japo baada ya talaka ilibidi Craid auze kampuni yake kwa USD 11 billioni , so now ana sihi maisha ya kawaida tuu akila bata ndogo ndogo
 
Number 2, Bernie na Slavica Ecclestone – $1.2 billion
huyu jamaa ana miliki vitu vifuatavyo Formula One Management, Formula One Administration, na ni part-owner of Alpha Prema, kamouni mama ya the Formula One Group of Companies. Bernie na Slavica Ecclestone walioana mwaka 1984
Lakin sku moja Slvica aliamka tuu na kusepa na watoto wake pia akenda kudai talaka, wana sema yeye alitaka pesa zaid ya hizo, sijui alitaka afanye talaka kama mgodi!!!!
Ila ndo hivo now ana kula bata tuu na mabilioni ya talaka hayo
 
Hahahaaa kweli Mungu hatakaaa awe jambilo au hata szczesny[emoji106]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…