Kufikia mwezi Septemba tutajua Usonji unasababishwa na nini..!
Waziri wa Afya wa Marekani, Robert F. Kennedy Jr. ameahidi kwamba katika kipindi cha miezi 5 ijayo serikali itakuwa inajua ugonjwa wa Usonji unasababishwa na kitu gani.
Waziri huyo amesema kwamba serikali itafanya tafiti kujua sababu za ugonjwa huo. Hata hivyo taasisi inayoshugulika na ugonjwa wa Usonji nchini humo imedai kwamba matamshi ya Waziri huyo ni hatari na ya kupotosha kwa sababu ni muda mfupi sana kufanya utafiti wa kubaini sababu za Usonji.
Mpaka sasa bado wataalam hawajajua Ugonjwa wa Usonji unasababishwa na nini. Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba sababu za kurithi na kimazingira zinaweza kuwa zinasababisha ugonjwa wa Usonji.
Matukio wa watoto wenye Usonji yameongezeka zaidi miaka ya karibuni. Huko nyuma Robert amewahi kudai kwamba Ugonjwa wa Usonji unasababishwa na chanjo, hata hivyo tafiti nyingi zimekanusha kwamba chanjo hazisabishi ugonjwa wa Usonji..!