Mganga alisema anataka macho ya mtoto, mama yake akamuuza mtoto wake kwa sangoma..!
Mahakama nchini Afrika Kusini imeelezwa kwamba Kelly Smith mama wa watoto watatu alimuuza mtoto wake kike Joslin Smith
kwa sangoma kwa sababu mtoto huyo alikuwa na macho pamoja na ngozi alivyokuwa anavitaka mganga kienyeji nchini humo.
Mwanamke huyo anashtakiwa na watu wengine wawili akiwemo aliyekuwa mpenzi wake kwa tuhuma za utakaji nyara na ulanguzi wa binadamu.
Polisi wanadai kwamba wakati wa msako wa kumtafuta mtoto wake mwanamke huyo alionekana kutojali na muda mwingi alikuwa akimuwazia tu mpenzi wake.
Mchungaji mmoja aliieleza mahakama kwamba, mwanamke huyo aliwahi kumwambia akipata mteja atauza watoto wake hata kwa Shilingi laki 7 hadi milioni 2.
Jirani wa mwanamke huyo alitoa ushahidi na kueleza kwamba, mwanamke huyo alimfuata na kumwambia amefanya jambo la kipumbavu kwa sababu amemuuza mtoto wake kwa sangoma.
Mtoto huyo alikuwa na macho ya bluu na ngozi ya kuvutia ambayo mganga alikuwa anavitafuta.
Bado mahakama haijaelezwa kwa nini sangoma alikuwa anahitaji macho ya rangi hiyo. Nchini Afrika Kusini waganga wa kienyeji huwa wanaitwa Sangoma.
Polisi nchini humo wanaamini kwamba kama mtoto huyo bado yuko hai basi atakuwa amesafirishwa kwenda mojawapo ya nchi za Afrika Magharibi..