Kwa watu wengi kuingia kwenye maji hayo yenye kiwango cha baridi kali ,Wakajikuta wakipata mshtuko wa ghafla na kupoteza uhai, wanasayansi wanadai vifo vingi vilitokana na mshtuko huo uliosababishwa na baridi pamoja na hali ya hofu iliyopelekea hata mafundi wa kuogelea kuzama, na waliojitahidi kuogelea walikufa kwasababu ya baridi kali lililotafuna miili yao ndani ya dakika chache.
Lakini hali ilikuwa ya tofauti kwa bwana Charles Joughin , mtaalamu wa kuogelea aliyelewa tilalila,aliweza kukaa zaidi ya masaa matatu kwenye maji ya barafu,
katika kiza kizito cha bahari ya Atlantic, ni makelele ya vilio vya watu waliokuwa wakifa ndiyo yaliyokuwa yakisika,bwana Joughin alikaa kwenye maji hayo hadi jua lilipoanza kuchomoza,ndipo akaogelea kusogelea boti aliloliona ,watu wakamshangaa walipomuona,na japokuwa hakukuwa na nafasi lakini wakamsaidia kwa kumshika mkono huku Miguu yake ikiwa ndani ya maji hadi msaada wa meli ya Caparthia ulipofika
Bwana Charles Joughin anakumbukwa kama mlevi aliyelishinda janga kubwa zaidi katika karne ya 20.