Farhan Jr
SIMBA IMEMPA MKONO WA KWAHERI CAPTAIN & LEGEND JONAS MKUDE
- Hii ni taarifa ya klabu kuwa imeachana na Mchezaji wake aliyeitumikia klabu kwa muda mrefu zaidi, ghafla ikaibuka agenda ya Mkude kutoagwa kwa heshima! Well ni agenda nzuri sana na wahoji wana hoja kubwa sana tena ya afya.
Lakini Uandishi wa Habari upo huru sana, linapokuja suala kama hili kuna pande mbili hapo ambao wote wanaweza kukupa ufafanuzi! Kuna JONAS MKUDE (Mchezaji) na SIMBA (Mwajiri wake wa zamani) hawa wote wanaweza kukupa majibu ya nini kifuatacho.
Nikalazimika kumpigia Afisa mmoja wa Simba jana usiku kumuuliza kuhusu suala la Jonas Mkude nae akanipa majibu yake juu ya hoja za watu wengi kama ifuatavyo.
Kaka taarifa ya Mkude kuagwa ndio mwisho pale? HAPANA, kwanza tumetoa taarifa kama inavyotakiwa hata EPL hutoa majina ya wachezaji wote wanaowaacha na wanaoendelea nao, sisi tumetoa majibu ya wachezaji tunaowaacha.
Nini kifuatacho? Ofcourse Jonas ni Mchezaji Mwandamizi na ameitumikia klabu kwa mafanikio makubwa sana, hivyo tutampa mwaliko maalum wa yeye kuja Simba Day na tutamuaga pamoja na Wanasimba.
- Mpaka sasa Simba wameaga kwenye hatua mbili! Cha kwanza taarifa rasmi ya klabu ambayo ipo Simba App, kisha video ya Mkude Jonas akiongea ambayo ipo Youtube pia akiappreciate na kuaga, hatua ya tatu ni uwanjani Simba Day kama ambavyo Afisa wa klabu alinipenyezea.
Ikumbukwe kuaga sio Kanuni bali utamaduni, Ulaya na Afrika baadhi ya klabu huishia press release pekee ila Simba wamesogeza mpaka video na Simba Day atapewa chance.
Huu ndio upande ambao haukuguswa ambao ndio upande wa Viongozi wa Simba ambapo wengi walikwepa kuwauliza na wakawapa majibu! Uandishi unaagiza sana kubalance vitu kwa pande zote.