The Gunners, Arsenal wanaripotiwa kupiga hatua kubwa kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na beki wake Mfaransa William Saliba ili isimpoteze kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi barani Ulaya.
.
Saliba alikuwa kwenye ubora mkubwa kwenye timu ya Arsenal msimu wa 2022-23 na jambo hilo limefanya klabu kibao kuhitaji saini yake ikiwamo mabingwa wa soka wa Ufaransa, Paris Saint-Germain.
.
Saliba aliumia Machi na kushindwa kuitumikia timu yake, lakini kabla ya kuumia alifunga mabao matatu na kuasisti mara moja katika mechi 33 na hakika aliunda kombinesheni matata kabisa na beki mwenzake Gabriel Magalhaes. Na sasa kocha Mikel Arteta anahangaika kuhakikisha kwamba anamsainisha mkataba mpya beki huyo ili kuepuka kusumbuliwa na timu nyingine zitakazohitaji saini ya mchezaji huyo.