Makapuku Forum

Mtangazaji Zamaradi Mketema leo amezindua na kuitambulisha TV yake ya Zamaradi ambayo itakuwa ikipatikana kupitia king’amuzi cha Azam TV kupitia channel number 413.

Zamaradi amesindikizwa na Mume wake Shabani ambaye ni Mshirika wake kwenye biashara hiyo Wake na baada ya uzinduzi Zama amezungumza na kusema “Sasa nitakuwa napatikana Mainstream, ni Entertainment Channel ambayo itakua na vipindi tofautitofauri, tumeingia rasmi tunaomba mtupokee”
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega leo amewasilisha Bungeni Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2023/ 2024 ambapo amesema katika mwaka 2022/2023, idadi ya mifugo nchini imeongezeka kutoka ng’ombe milioni 35.3 hadi ng’ombe milioni 36.6, mbuzi kutoka milioni 25.6 hadi milioni 26.6 na kondoo kutoka milioni 8.5 hadi milioni 9.1.

“Kuku pia wameongezeka kutoka milioni 92.8 hadi milioni 97.9 ambapo kuku wa asili wameongezeka kutoka milioni 42.7 hadi milioni 45.1, kuku wa kisasa kutoka milioni 50.1 hadi milioni 52.8 na nguruwe kutoka milioni 3.4 hadi milioni 3.7, aidha ukuaj wa Sekta ya Mifugo kwa mwaka 2021 umefikia asilimia 5.0 na kuchangia asilimia 7.0 kwenye Pato la Taifa”

“Katika mwaka 2022/2023 ng’ombe 2,218,293 na mbuzi/kondoo 2,121,187 wenye thamani ya Shilingi trilioni 1.7 waliuzwa katika minada mbalimbali hapa nchini ikilinganishwa na ng’ombe 2,194,937; mbuzi/kondoo 1,782,010 wenye thamani ya Shilingi trilioni 1.5 waliouzwa katika mwaka 2021/2022”
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega leo amewasilisha Bungeni Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2023/ 2024 ambapo amesema uzalishaji wa nyama umeongezeka kwa 4.3% kutoka tani 769,966.7 mwaka 2021/2022 hadi tani 803,264.3 mwaka 2022/2023 huku uzalishaji wa maziwa ukiongezeka pia kutoka lita bilioni 3.4 mwaka 2021/2022 hadi kufikia lita bilioni 3.6 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la 5%.

Ulega amesema “Vipande vya ngozi milioni 14.1 vimezalishwa mwaka 2022/2023 ikilinganishwa na vipande milioni 13.6 vilivyozalishwa mwaka 2021/2022, uzalishaji wa mayai umeongezeka kutoka mayai bilioni 4.9 mwaka 2021/2022 hadi bilioni 5.5 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la 12.2%”

“35% ya kaya zilizopo nchini zinajishughulisha na ufugaji, kati ya hizo 39.3% wanafuga ng’ombe, 36.2 % wanafuga mbuzi, 13.5% wanafuga kondoo na 10.9% wanafuga nguruwe, aidha 55.4% ya kaya hizo pia hujishughulisha na ufugaji wa kuku”
 
Wafuasi wa Chama cha Azimio la Umoja kinachoongozwa na Raila Odinga wameendelea na maandamano asubuhi hii kama walivyotangaza licha ya Rais wa Kenya William Ruto kusema yupo tayari kutumia Mamlaka aliyonayo kama Amiri Jeshi Mkuu kuzuia maandamano hayo.

Miongoni mwa matukio yaliyoshuhudiwa asubuhi hii ni kuchomwa kwa basi na matairi Barabarani, itakumbukwa juzi Ruto alisema amejaribu kuwaambia Odinga na Wafuasi wake wasiandamane ila wamekataa hivyo akaahidi kwamba wakilazimisha kuandamana watajua hawajui.

Akiongea akiwa eneo la Malava Kaunti ya Kakamega, Ruto alinukuliwa akisema “Nilimuita Odinga nikamuomba asitishe maandamano, wamekataa, Mimi niliwaambia ile wiki nyingine, nikaita yule Mzee wa kitendawili na nikamwambia wewe wacha hii maandamano tupeleke hii maneno yote unasema Bungeni, Wabunge waangalie kama kuna maneno ya ukweli”

“Sasa eti wamekataa hiyo ya kwenda kuongea kwa amani Bungeni, eti wanataka kurudia maandamano, eti waende wavunje mali na kuharibu biashara ya Wananchi, Mimi ndio commander-in-chief, nyinyi mtajua hamjui, waache hiyo mchezo”
 
Waziri wa Kazi, Ajira na Uhusiano wa Viwanda Nchini Uganda, Charles Okello Engola ameuawa asubuhi hii kwa kupigwa risasi na Mlinzi wake (Bodyguard), Spika wa Bunge la Uganda Anitha Among amethibitisha Bungeni leo.

Tukio hilo limetokea asubuhi hii ambapo imeripotiwa kuwa Waziri Okello alikuwa anatoka nyumbani kwenda kazini ambapo ghafla Mlinzi wake alimpiga risasi kisha akaanza kupiga risasi juu huku akikimbiakimbia Mtaani, Majirani wamesema Mlinzi huyo alisikika akisema hajalipwa mshahara kwa muda mrefu licha ya kufanya kazi na Waziri huyo.

Inaripotiwa kuwa Mlinzi huyo baadaye aliingia Saluni moja iliyopo Jirani na nyumba ya Waziri kisha akawataka waliokuwa ndani kutoka nje na akajifungia na kujipiga risasi na kufariki pia.
 
Katika hali ya kushangaza, uchunguzi (autopsy) uliofanywa kwa miili 110 ya waliokuwa waumini wa Kanisa la Good News International linaloendesha shughuli zake katika Msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi nchini Kenya, umebaini kuwa, baadhi ya waathiriwa waliuawa kwa kukosa hewa na kunyongwa.

Zoezi la uchunguzi huo lilifanyika katika chumba cha hifadhi ya maiti cha Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Malindi, lililoongozwa na Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali Johansen Odor na kubaini viashiria kwa watoto wawili walifariki kwa kukosa hewa kutokana na kuzibwa mdomo na pua.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Nation uliomnukuu Mwanapatholojia huyo, katika zoezi hilo la uchunguzi lililofanyika jana Mei 1, mwaka huu timu hiyo ilifanikiwa kuchunguza miili ya watoto tisa wenye umri kati ya mwaka mmoja na nusu hadi kumi na mwanamke mmoja.

 
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatarajia kuanzisha Mamlaka za Uvuvi pamoja na ile ya Mifugo kwa ajili ya kukusimamia na kuendeleza miundombinu ya sekta hizo mbili muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Waziri wa wizara hiyo Abdallah Ulega amelieleza Bunge leo Jumanne Mei 2, 2023 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka mpya wa fedha 2023/2024 ambapo, amesema hatua hiyo inalenga kusogeza karibu huduma kwa wadau wa sekta hizo na kuongeza tija.

Amesema kwa sasa mchakato huo upo kwenye hatua ya kufanya tathimini kwa wadau kwa kukusanya maoni na kwamba, changamoto zote zitakuwa zikipatiwa ufumbuzi kupitia kwenye mamlaka hizo.
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kuwa katika mwaka mpya wa fedha 2023/2024 Serikali itaanzisha skimu za umwagiliaji katika mashamba ya Vikunge, Langwira na kwenye Ranchi za Taifa za Kongwa na Mzeri.

Pia, imepanga kujenga mabwawa na visima virefu kwa ajili ya maji ya mifugo na kuanzisha mashamba darasa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Waziri Ulega ameeleza hayo leo Jumanne Mei 2, 2023 wakati akiwasilisha makadario ya mapato na matumizi bungeni kwa ajili ya wizara yake kwa mwaka mpya wa fedha. Mkakati huu ni sehemu ya vipaumbele vya wizara hiyo.
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Serikali itaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa Bandari ya Uvuvi iliyopo Kilwa Masoko mkoani Lindi na kwamba, itakapokamilika itasaidia kuongeza tija kwenye shughuli za uvuvi nchini.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo bungeni mjini Dodoma leo Jumanne, Mei 2, 2023 Ulega amesema tayari ujenzi huo unaendelea na kwamba, itakapokamilika itaongeza thamani kwa wavuvi hivyo, kukuza vipato vyao na kuchangia mapato ya Serikali.

Sambamba na ujenzi wa bandari hiyo, Ulega amesema kuwa Serikali imenunua meli tatu za uvuvi wa Bahari Kuu, kufanya utafiti wa wingi wa mtawanyiko wa samaki na kutoa leseni kwa meli za uvuvi wa Bahari Kuu.

 
Wafuasi wa Chama cha Azimio la Umoja kinachoongozwa na Raila Odinga nchini Kenya wameendelea na maandamano leo kama walivyotangaza licha ya Rais William Ruto kusema yupo tayari kutumia mamlaka aliyonayo kuzuia maandamano hayo.

Baadhi ya matukio yaliyoshuhudiwa asubuhi hii ni kuchomwa kwa basi katika barabara ya Ngong na kuchoma matairi.

Akizungumza akiwa eneo la Malava Kaunti ya Kakamega, Rais Ruto alinukuliwa akisema “Nilimuita Odinga nikamuomba asitishe maandamano, wamekataa, mimi niliwaambia ile wiki nyingine, nikaita yule mzee wa kitendawili na nikamwambia wewe wacha hii maandamano tupeleke hii maneno yote unasema bungeni, wabunge waangalie kama kuna maneno ya ukweli”

“Sasa eti wamekataa hiyo ya kwenda kuongea kwa amani bungeni, eti wanataka kurudia maandamano, eti waende wavunje mali na kuharibu biashara ya Wananchi. Mimi ndio commander-in-chief, nyinyi mtajua hamjui, waache hiyo mchezo.”

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…