Makapuku Forum

Kikosi cha Rivers United ya Nigeria kimeanza safari kuja Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kucheza mechi ya pili robo fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga katika Uwanja wa Mkapa Aprili 30.

Mechi ya kwanza timu hiyo ilifungwa mabao 2-0 yakiwekwa wavuni na Fiston Mayele.
 
Kesho Ijumaa Aprili 28 pale jijini Casablanca, Morocco saa 1 usiku sawa na saa 3 usiku Tanzania, wawakilishi wa
Ligi ya Mabingwa Afrika watakuwa uwanja wa Mohammed V kusaka tiketi ya kwenda nusu fainali dhidi ya Wydad.

Simba tayari ishaanza mazoezi huku kocha msaidizi wa timu hiyo Juma Mgunda amesema wachezaji wote wapo vizuri kwa ajili ya mchezo huo.

Mgunda amesema nyota wao Moses Phiri ambaye aliumia mechi dhidi ya Kagera Sugar yupo fit kwasasa baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwasababu jeraha lake lilikuwa kubwa.

 
DAKTARI wa Kagera Sugar, Abel Shindika amesema kitendo cha beki wa timu hiyo, Datius Peter kuzimia ni jambo la kawaida kwa mchezaji yeyote kutokana na utumiaji wa nguvu pindi anapotimiza majukumu uwanjani.

Beki huyo wa kulia alizimia ghafla uwanjani baada ya kugongana na mshambuliaji wa Mbeya City, Sixtus Sabilo dakika ya 38 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Aprili 23 kwenye Uwanja wa Kaitaba na wenyeji kushinda bao 1-0.

Akizungumza na Mwanaspoti, Shindika alisema nyota huyo alipata mshtuko baada ya kugongwa sehemu ya goti lake kwa nyuma hivyo kumsababishia kupoteza fahamu ila baada ya kufanyiwa vipimo amegundulika hana tatizo lolote.

"Tulimpima pale pale uwanjani lakini baada ya hapo tukampeleka hospitali ya karibu kwa ajili ya matibabu zaidi na tukagundua alipata mshtuko mdogo tu ambao hauna madhara yoyote hivyo anaendelea vizuri kwa sasa," alisema.
 
Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi ameliambia Mwanaspoti amefanya kikao maalumu na wachezaji wake kabla timu yao haijaanza safari ya kuondoka nchini Nigeria na ujumbe wake mkubwa ni wafute matokeo ya ushindi wa kwanza.

Nabi alisema licha ya timu yake kushinda ugenini lakini bado wapinzani wao wanahitaji kuheshimiwa kutokana na ubora wao ambao wanaweza kuja kupindua matokeo endapo watawadharau.

"Nimewaambia wachezaji wangu furaha ya ushindi iliishia pale geti la uwanja tulioutumia kucheza ile mechi, sitaki kuona mchezaji yeyote akiendelea kufurahia ule ushindi, ile mechi imekwisha, ni sawa na tumecheza dakika 45 za kipindi kimoja na hapa tunakuja kucheza dakika 45 za kumalizia mchezo," alisema Nabi

"Huu ujumbe wangu naomba pia uwafikie mashabiki wetu, wajue kazi haijamalizika, kama tukifanya makosa ya kujisahau tunaweza kuja kupata mshtuko mbaya, tunatakiwa kushinda haraka katika mchezo ujao Jumapili,"

Yanga itarudiana na Rivers United Jumapili Aprili 30 katika uwanja wa Mkapa kusaka tiketi ya nusu fainali Kombe la Shirikisho.
 
SAA 24, tangu tiketi za mchezo wa Simba na Wydad Casablanca sambamba na ule wa Raja Casablanca na Al Ahly ziwekwe sokoni, tiketi hizo zimeuzwa zote huku mashabiki wakitakiwa kulipa Sh 160,000 ili kumwona Jean Baleke akiwa uwanjani.

Michezo hiyo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa inatarajiwa kupigwa wikiendi hii na mwakilishi wa Tanzania, Simba itakuwa kwenye Uwanja wa Mohammed IV, Ijumaa Aprili 28, kuivaa Wydad huku Raja ikivaana na Al Ahly Aprili 29, kwenye uwanja huo huo.

Kiingilio cha chini cha mchezo kati ya Wydad na Simba ambayo ina mastaa wakubwa, Clatous Chama na Jean Baleke wenye mabao manne kila mmoja kwenye michuano hiyo, ni Dirham 30, sawa na Sh6,000 za Kitanzania, huku kiingilio cha juu ni Dirham 700 (Sh160,000).

Moja ya silaha kubwa za Raja na Wydad ni mashabiki wao wanaojitokeza kwa wingi hususan kwenye mechi muhimu kama hizo na hushangilia kwa nguvu zote kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo bila kujali matokeo.

 
Chelsea wamethibitisha kuwa Frank Lampard ataendelea kuwa na timu hiyo kama Kocha wa muda mpaka mwishoni mwa msimu, kifupi ni kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumtimua.
 
Farhan Jr

Nimewaona Makocha wengi sana duniani, nimeupenda mpira na kuwatazama wakifanya mambo mengi sana ila kwangu PEP GUARDIOLA ndie Kocha bora kuwahi kumshuhudia akifundisha Kabumbu.

THE GREATEST OF ALL TIME, MASTER PEP GUARDIOLA.
 
Farhan Jr

Pep Guardiola anauishi sana mpira, aliwahi kumnasa kibao Kijana wake Thiago Alcantara pale Bayern Munich, aliwahi kumtoa Zlatan Ibrahimovich pale Barcelona kisa kutofuata maelekezo, Master anauishi sana mpira kuliko kawaida.

Jana imemtokea Ederson wakati wanashangilia bao la kwanza akageuka chaap na kumwita Ederson ambaye ni Golikipa na kuanza kumpa maelekezo kwenye touchline.

Baada ya goli kufungwa la kwanza kufungwa na KDB, Pep Guardiola alishangilia kisha ghafla sana akamwita Golikipa Ederson na kumlaumu, wengi hatukufahamu sababu.

Kumbe Ederson alipaswa kumpa mipira yote Rodri ambaye ana vision ya kujua nani yupo free na ampe pass ili waondoke kwenye press ya Arsenal, sasa Golikipa akacheza na Stones ambaye alikuwa na presha kubwa.

Bahati ni kuwa Stones alipiga mpira mrefu uliofika kwa Halaand akacheza na KDB, lakini Pep ilibidi amkumbushe Kipa wake na kuanzia hapo akaanza kucheza na Rodri kama mpango wake.

Huyo ndio Pep! Ndio tumepata goli ila sio kama ambavyo mipango yangu inataka


THIS IS PEP GUARDIOLA.

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…