Makapuku Forum

Urusi imekataa ombi la Balozi wa Marekani Nchini humo la kumtembelea gerezani Mwandishi wa Habari wa Marekani Evan Gershkovich anayezuiliwa nchini humo kwa tuhuma za kijasusi.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema wamefanya hivyo kuijibu Marekani ambayo imewanyima Waandishi wa Habari wa Urusi vibali vya kuingia Nchini kwake (VISA) ambao walitakiwa kuambatana na Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov anayekwenda kuhudhuria kikao cha Umoja wa Mataifa New York.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili, Ikulu, Dar es Salaam tarehe leo April 27 Aprili, 2023.

Rais Kagame yupo nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.
 
Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wameongea na Waandishi wa Habari leo baada ya kufanya mazungumzo yao, Ikulu, Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine Rais Samia amesema ziara hiyo ya Kagame ni fupi lakini yenye mafanikio makubwa.

Rais Samia amenukuliwa akisema “Tumepata ziara tulikuwa tukiisubiri kwa siku nyingi, Kagame anasema ziara fupi lakini bora nimekuja kuliko nisingekuja, ni ziara fupi lakini yenye mafanikio, ziara imetupa muda mzuri wa kutathmini masuala ya ushirikiano”

"Katika mazungumzo yetu kuna mambo tumeyafanyia kazi lakini hatujamaliza kwahiyo tumekubaliana Nchi zote mbili zikafanyie kazi kila moja na upande wake halafu Watalaamu wetu wakutane na watuambie wamefikia wapi"

"Katika masuala ambayo tumejadili, kuhusu biashara tumeona haja ya kukuza biashara na kuweka miundombinu ya kukuza biashara, nimempa taarifa Mh.Kagame kwamba Tanzania sasa tunafanya kazi kuimarisha Bandari zetu hasa Tanga na Dar es salaam ambazo Rwanda wanazitumia"

"Tumezungumzia pia suala la mradi wetu wa Rusumo ambao unakwenda vizuri na tumekubaliana tutakwenda kuuzindua kwa pamoja tumekubaliana vyombo vyetu vya usalama viendelee kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha usalama katika Nchi zetu na ukanda wetu wa Afrika Mashariki"
 
Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wameongea na Waandishi wa Habari leo baada ya kufanya mazungumzo yao, Ikulu, Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine Rais Kagame amesema Tanzania ni Mshirika mkubwa wa Rwanda.

Rais Kagame amenukuliwa akisema “Asante Dada yangu Samia Suluhu Hassan kwa kuniwezesha kufika kwa ajili ya ziara hii ambayo ni fupi, mambo muhimu umeyasema Mimi nitazungumza kwa ufupi sana, naomba uniruhusu nitumie Kiingereza, ingawa najitahidi kuzungumza Kiswahili kizuri ningependa kuzungumza Kiswahili kizuri kama chako lakini bado kazi inahitajika"

"Mimi na Rais Samia tulikuwa na mazungumzo na tumekubaliana kudumisha uhusiano zaidi wa kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kihistoria, Tanzania na Rwanda zina mzizi mzuri wa ushirikiano wa muda mrefu"

"Tanzania ni Mshirika mkubwa wa Rwanda hususani kwenye upande wa biashara, tunaheshimu kitendo cha Tanzania kukubali kudumisha zaidi ushirikiano huu kwa faida za Mataifa yote mawili ili kuruhusu Watu wetu kupata maendeleo ya haraka na Kampuni zetu kushindana vizuri kwenye Masoko ya Kimataifa"

"Mwisho Mh.Rais Samia nakushukuru kwa Uongozi wako katika kutafuta suluhisho la kudumu kwenye mgogoro ambao upo kwenye Kanda yetu ya Afrika Mashariki hususani mgogoro tunaoshughulika nao Mashariki ya Congo, ukishirikiana na Viongozi wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki"

"Kujenga amani ya kudumu na usalama kwenye Ukanda wetu tunahitaji kujitoa na kuwa na msimamo imara kwetu sote ikiwemo wale ambao wameathirika moja kwa moja na mgogoro huu, amani na utulivu ni hitaji muhimu sana kwa ajili ya maendeleo na umoja wa Afrika, Mh.Rais kwa mara nyingine tena nakushukuru kwa mapokezi mazuri yanayotufanya tujisikie tuko nyumbani, asanteni sana
 
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imefanikiwa kuwaondoa Nchini Sudan Wanafunzi wote wa Kitanzania wanaosoma huko na kuwarejesha Tanzania ili kuokoa maisha yao kufuatia vita inayoendelea nchini humo.

Safari ya kurejea nyumbani ilianzia Khartoum kwa mabasi saa 7.30 mchana ya April 24, 2023 na kuelekea Mji wa Al Qadarif ambao upo takriban kilometa 420 kutoka Mji Mkuu wa Khartoum ambapo msafara ulifika Al Qadarif usiku na kulazimika kulala kutokana na usalama na kuondoka asubuhi ya tarehe 25 April 2023 kulekea Mji wa Metema, Ethiopia ambao unapakana na Sudan kisha kuelekea Mji wa Gondar, Ethiopia.

Watanzania hao 206 wakiwemo Wanafunzi 170, Maafisa wa Ubalozi na Wakazi wengine walisafiri kwa ndege kwenda uwanja wa Bole, Addis Ababa kisha wakachukuliwa na Ndege ya Tanzania (ATCL) dreamliner kuja Dar es salaam ambapo wamepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje Dr. Tax.
 
Wanajeshi wa Ujerumani wanakaribia kuondoka kwenye Taifa la Mali Barani Afrika ikiwa ni miaka 7 tangu Ujerumani itume Wanajeshi zaidi ya elfu moja kulinda amani kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali ambapo walitakiwa kusaidia kurejesha utulivu nchini humo lakini wameamua kuondoka kwa sababu Serikali ya Kijeshi ya Mali haijawapa ushirikiano.
 
Serikali ya Singapore imemnyonga hadi kufa Raia wake aitwae Tangaraju Suppiah (46) hapo jana kama adhabu ya kupatikana na hatia ya kusafirisha kilo moja ya dawa za kulevya aina ya bangi mwaka 2018 ambapo Dada yake amesema tayari familia yao imekabidhiwa cheti cha kifo chake.

Ingawa matumizi ya bangi yameendelea kuhalalishwa katika Mataifa mbalimbali duniani, Nchi ya Singapore bado inashikilia baadhi ya misimamo yake ya sheria kali zaidi za dawa za kulevya na kusisitiza kwamba adhabu ya kifo inafanya kazi vizuri kuwazuia wasafirishaji wa dawa za kulevya ambapo chini ya sheria za Nchi hii Mtu yeyote anayepatikana akisafirisha, kuingiza au kusafirisha kiasi fulani cha dawa za kulevya kama vile methamphetamine, heroini, cocaine au bidhaa za bangi atapokea hukumu ya kifo.

Siku chache kabla ya Tangaraju kunyongwa, Wanafamilia na Wanaharakati walimuombea msamaha hadharani huku Ofisi ya Umoja wa Ulaya katika jimbo la Jiji hilo na Ofisi ya haki za Umoja wa Mataifa zikitoa wito kwa Singapore kutotekeleza hukumu hiyo, juhudi ambazo hata hivyo hazikufanikiwa.
 
Polisi Nchini Kenya wamesema maiti za Waumini wa Kanisa la Good News International Church linaloongozwa na Mchungaji Paul Mackenzie, ambaye anashikiliwa na Polisi kwa madai ya kuwataka Waumini wake kufa njaa ili kufika Mbinguni kwa haraka, zimefikia 98.

@dw_kiswahili wameripoti kuwa miili kadhaa imepatikana ikiwa imezikwa kwenye makaburi katika msitu wa Shakahola karibu na Mji wa pwani wa Malindi huku Kiongozi wa Kanisa la Good News International, Paul Mackenzie Nthenge akituhumiwa kuwarubuni Wafuasi wake kwa kuwaaminisha kwamba njaa ndiyo njia pekee itakayowapeleka kwa Mungu.

Sakata hilo la kutisha ambalo limepewa jina la "Mauaji ya Msitu wa Shakahola", limesababisha Watu kutoa wito wa kukaguliwa kwa Madhehebu ya kidini katika Nchi ya Kenya hiyo yenye Wakristo wengi.
 
Kampuni ya moja ya Korea Kusini iitwayo Hana Financial Group imetangaza kutoa bure kumbi na maeneo yake kwa ajili ya Maharusi wapya kufanya sherehe zao ikiwa ni sehemu ya mpango wa kusaidia kuongeza kiwango cha Watu kuzaliana nchini Korea ambacho kimekua ni janga la Taifa.

Jitihada za kuhamasisha Watu kuzaliana ni jitihada za Taifa zima na tayari Serikali imetumia zaidi ya dola bilioni 200 katika kipindi cha miaka 16 iliyopita ili kuongeza kiwango cha kuzaliana lakini imeshindwa kugeuza wimbi hilo na kushuhudia hata wastani wa Mwanamke kujifungua nchini humo ukifikia 33.5 hadi mwaka 2022.

Takwimu za hivi karibuni pia zilionyesha kuwa kwa mwaka 2022 Nchi nzima walizaliwa Watoto 249,000 tu tena idadi ikiwa imepungua kutoka Watoto 260,000 waliozaliwa mwaka 2021 katika Nchi hiyo ambayo hadi mwaka 2020 ilikua na jumla ya Watu milioni 51.84 na ikashuka hadi milioni 51.74 mwaka 2021 na ifikapo mwaka 2070 Nchi hiyo inatarajiwa kuwa na idadi ndogo zaidi ya Watu ya milioni 37 pekee.
 
Polisi nchini Kenya katika Kaunti ya Kilifi wamemkamata mchungaji mwingine anayejulikana kwa jina la Ezekiel Odero kwa tuhuma za kuhusika na vifo vya waumini katika Kanisa lake linalojulikana New Prayer Centre.

Tukio hilo limetokea katika Kaunti ya Kilifi siku chache tangu kuibuliwa mauaji ya waumini wa kanisa linaloongozwa na Mchungaji Paul Mackenzie ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi.

Kamanda wa Polisi Kanda ya Pwani, Rhoda Onyancha amenukuliwa akisema, “Tumemkamata Mchungaji Ezekiel wa Kanisa la ‘New Prayer Centre’ kwa tuhuma za kuhusika na vifo ambavyo vimekuwa vinatokea katika eneo lake.

 
JOYCE LOMALISA MUTAMBALA, SIJUI KWANINI ILA SITAMANI UTAMU UISHE.

Ni katikati ya marehemu Christian Atsu, miguu ya fundi Issama Mpeko na Mido Wakaso Mubarak ulipigwa mpira mrefu kutoka alipo golikipa wa Congo Ley Matampi kisha ukawavuka ndugu wawili Jordan na Andre Ayew, tayari Ball Boy mmoja alishajivuta kuuokota ule mpira unaoelekea kutoka nje Chancel Mbeba na kasi yake yote alishakata tamaa mpira ulikuwa mrefu sana

Wakati Line One akijiandaa kuamuru mpira wa kurushwa kuelekea lango la Congo, zilisikika sauti za shangwe za wendawazimu na vichaa wa soka kutoka kwenye jukwaa moja la VIP pale dimbani Stade Oyem, sijui nini kiliendelea ila nachokumbuka tayari mpira ulikuwa umetulia chini ya mguu wa kushoto wa Joyce Lomalisa Mutambala. Afcon 2017 Congo dhidi ya Ghana.
 
ONANA KUMUONDOA KEPA CHELSEA
.
Chelsea inataka kumtumia kipa Mhispania Kepa Arrizabalaga kama sehemu ya ofa ya kumsajili kipa wa Inter Milan na Cameroon, Andre Onana, 27 katika dirisha lijalo.
.
Mabosi wa Chelsea wanataka kumsajili Onana kutokana na upungufu ambao umeonyeshwa na Kepa kwa msimu huu ambapo amekuwa na makosa mengi.
.
Onana ambaye msimu huu anaongoza kwa saves (40) na clean sheet (6) katoka Ligi ya Mabingwa Ulaya , amekuwa mhilimili muhimu kwenye kikosi cha Inter ambacho amekisaidia kufuzu hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.
.
Mkataba wa sasa wa kipa huyo unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, na mabosi wa Inter wanadaiwa kuhitaji kiasi kisichopungua Pauni 35 milioni ili kumuuza.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…