Makapuku Forum

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Dominic Raab amejiuzulu baada ya ripoti ya uchunguzi kuthibitisha madai kuwa aliwanyanyasa waliokuwa chini yake.

Hata hivyo amekanusha madai hayo akisema alitekeleza majukumu yake kwa weledi wakati wote.
 
Mwanzilishi wa Twitter, Jack Dorsey ni miongoni mwa watu mashuhuri duniani ambao alama ya uthibitisho imeondolewa kwenye akaunti zao baada ya Elon Musk kuleta utaratibu wa kulipia.

Papa Francis, Beyonce, Bill Gates, Rais Trump ni miongoni mwa wengi walioondolewa alama hizo.
 
Takriban watu 78 wamefariki katika mkanyagano uliotokea katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a wakati wa ugawaji wa chakula cha msaada kwa ajili ya Ramadhan.

Tukio hilo limetokea Jumatano jioni wakati mamia ya watu walipomiminika katika shule moja wilaya ya Bab al-Yemen mjini Sana’a kwa ajili ya kupata msaada wa takribani dola 10 [TZS 23,460] ambazo zilikuwa zikitolewa na wafanyabiashara kwa ajili ya kuadhimisha siku za mwisho za Ramadhani.

Video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha watu wakipiga mayowe huku wengine wakiwa chini wakijaribu kuomba msaada, baadhi yao wakiwa hawatikisiki na wengine wakijaribu kutoa msaada.

Mashahidi wameiambia shirika la habari la Associated Press kwamba watu waliokuwa na silaha walifyatua risasi hewani katika kujaribu kudhibiti umati wa watu na kisha waligonga waya wa umeme ambao ulilipuka na kusababisha hofu miongoni mwa waliokuwa wakisubiri.

Wafanyabiashara mjini humo ambao walipanga tukio hilo la utoaji wa misaada wamekamatwa na uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo, imesema wizara ya mambo ya ndani.
 
Daah njaa mbaya
 
Naaaaaaam...
Na Kazi Iendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…