Nchi za Ufaransa, Italia na Marekani zimekuwa vinara wa kuleta wageni wengi wa kimataifa nchini katika kipindi cha Januari hadi Februari 2022 kutoka nje ya Afrika.
Huku kwa nchi za ndani ya Afrika, Kenya na Burundi zikiongoza. Hata hivyo katika kipindi hicho watalii wa kimataifa wameongezeka kwa asilimia 49 mwaka huu ikilinganishwa na mwaka 2022.
“Wageni wa kimataifa wamefika 290,896 mwaka huu katika kipindi cha Januari na Februari kutoka wageni 195,483 mwaka 2022 katika kipindi kama hicho.” Imesema ripoti ya NBS.
Katika ripoti iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inaonyesha kwa nchi Ufaransa iliongoza kuleta watalii 25,837 ikifuatiwa na Italia iliyoleta watalii 18,556 na Marekani walikuwa 16,567.
Nchi nyingine ni Ujerumani (15,705), Poland (12,369) na Uingereza (10,657). Kwa upande wa nchi za Afrika, Kenya inaongoza kwa kuleta watalii 29,615 ikifuatiwa na Burundi (16,832), Rwanda (7,627) na Malawi (6,563).
Nchi nyingine ni Uganda (6,511) na Afrika Kusini ilileta watalii 5,196.