#VituExtra.
MWENYE HEKIMA NA KUHESHIMIKA ZAIDI - ACHRAF HAKIM.
Duniani kote kuna asili ya majina na maana zake. Mara nyingi kama sio mara zote kuna baadhi ya majina hubeba ‘Kusudio na suluhisho’
Jina la ACHRAF lina maana ya ‘Anaeheshimika zaidi’ na Hakim maana yake ‘Hekima’. Nmetoa hizi tafsiri kwenye lugha ya kiarabu.
Kwenye michezo story kubwa leo hii ni kuhusu nyota wa PSG, Beki wa kupanda na kushuka Achraf Hakim kwa jinsi ambavyo amecheza kama “Pele” kwa Ex-wife wake Hiba Abouk.
Achraf huu ni wakati wake wa kutumia zaidi Hekima na kutunza heshima yake. Kwanini?
Feb 24, 2023 Zilitoka taarifa kuwa mwamba akiwa kwenye hekalu lake huko Paris alishikwa na upwiru uliomkaba koo akamrukia mdada mwenye umri wake miaka 24, na inasemakana Achraf alibaka.
Lakini wakati zinatoka hizi taarifa za Achraf kubaka, mkewe alitoka hadharani na kusema wakati huo walikua tayari wameshaachana na Achraf. Mke alimkana mumewe SAA SITA KAMILI JUA KALI na aliongeza kwa kusema hawezi hata siku 1 hawezu kuwa upande wa WABAKAJI.
Mahakamani, Achraf alikana mashitaka, kesi bado ipo kwenye uchunguzi, na PSG walisema wanamuamini mchezaji wao na hawakumtema kikosini.
Fast forward, 14 April 2023 Leo zinatoka taarifa kuwa Achraf hakim ameshinda kesi dhidi ya mzazi mwenzake kwenye suala la kugawana mali.
Taarifa zinasema Achraf mali zote alizisajili kwa jina la mama yake mzazi, hvyo mke wa Achraf hana chake cha kuchukua kutoka kwa Achraf. Watu wa kubet hii mnaitaje? NO GG, au sio?
Lakini tukumbuke kesi ya Achraf ya kubaka bado inafanyiwa uchunguzi, na aliebakwa anasema ana ushahidi wote.
Hakim kama ilivyo maana ya jina lake ‘Hekima’ imemuwezesha kushinda mtego wa kwanza wa ndoa na kulinda mali zake. Je mtego wa pili wa kubaka, Ataweza kushinda kesi na kulinda Heshima ya jina lake la Achraf lenye maana ya anayeheshimika zaidi?
LETS WAIT AND SEE[emoji817]