Makapuku Forum

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo February 13, 2023 kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada katika Shule za umma na binafsi nchini.

Vitabu vya 16 vilivyopigwa marufuku vimekutwa katika baadhi ya Shule si kama vitabu vya kiada wala ziada ambapo maudhui yake yanakinzana na mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania na yanahatarisha ukuaji wa Wanafunzi ikiwemo vinavyofundisha mapenzi ya jinsia moja.

Vitabu vilivyopingwa marufuku kutumika na kuwepo shuleni ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid - The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever.

Vingine ni Diary of a Wimpy Kid - The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid - Hard Luck, Diary of a Wimpy Kid - The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway, Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode.

Vitabu vingine vilivyopigwa marufuku kutumika shuleni ni Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.
 
Wananchi wa Kijiji cha Tangazo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara wamekumbwa na taharuki mara baada ya kuvamiwa na mnyama (Kiboko) akitoka eneo la jirani la Kijiji hicho.

Wananchi hao wamesema kwa sasa wanashindwa kufanya shughuli zao za kilimo kwakuwa Kiboko huyo yupo karibu na eneo la mashamba yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Tangazo Salumu Mtolia amesema kuwa kijijijni hapo hakuna madhara yaliyojitokeza kwa Wananchi hadi sasa licha ya Kiboko huyo kuwatishia Wananchi wanaoenda shambani Kwa shughuli zao za kilimo.

Mwenyekiti huyo ametoa wito Kwa Idara inayohusika na wanyamapori hapa nchini kutembelea eneo hilo ili waweze kumuondoa Kiboko huyo na Wananchi wake waweze kuwa huru kwenye shughuli zao za kilimo.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo February 13, 2023 ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Songwe ambapo akiwa katika kijiji cha Kaloleni kata ya Mkwajuni ameweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya ya Songwe.

Ujenzi wa Hospitali hiyo ambao umegharimu shilingi bilioni 3.5 mpaka sasa imefikia asilimia 95 ya ujenzi wake ambapo Halmashauri inatarajia kukamilisha mradi huo tarehe 31 machi 2023, ikiwa ni sambamba na kuanza kutumika rasmi kwa majengo yote ambayo
tayari vifaa vyake vimepokelewa.

Ujenzi katika Hospitali hiyo unahusisha ujenzi wa majenho ya huduma za Wagonjwa wa nje, mionzi, maabara, ufuaji, famasia, utawala na jengo la Mama na Mtoto na ujenzi wa wodi tatu za Magonjwa mchanganyiko.

Majengo mengine ni jengo la huduna ya dharura na nyumba ya Watumishi Familia tatu, jengo la upasuaji, jengo la uchunguzi na kuhifadhia maiti na wodi mbili za upasuaji (Wanaume na Wanawake)

Majaliwa amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amehakikisha hakuna eneo katika nchi hii ambao hapajatekelezwa miradi ya huduma za jamii kuanzia ngazi ya Mkoa hadi kijiji.
 
Ripoti mpya ambayo imewekwa kwenye tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (@tcra_tanzania ) imeonesha kwamba Mtandao wa Facebook ndio unaoongoza l kwa kuwa na idadi kubwa ya Watumiaji nchini Tanzania kuliko Mtandao mwingine wowote.

Mpaka December 2022 Facebook imeongoza kwa kutumia data GB Trilioni 90.01 ikifuatiwa na YouTUBE GB Trilioni 34.97, WhatsApp GB Trilioni 31.67, TikTok GB Trilioni 21.95 na Instagram GB Trilioni 13.43.

Kwa upande wa laini za simu zinazotumika Nchini, kuna ongezeko la 4% ambapo September 2022 kulikuwa na laini milioni 58.1 lakini hadi December 2022 laini ziliongezeka na kufikia milioni 60.3.
 
Ripoti mpya ambayo imewekwa kwenye tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (@tcra_tanzania ) imeonesha kwamba Mkoa wa Dar es salaam unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya laini za simu zinazotumika ( zipo ‘active’) kuliko Mkoa mwingine wowote Nchini Tanzania.

Mpaka December 2022 Dar es salaam imeongoza kwa kuwa na laini milioni kumi na laki nne na elfu hamsini na saba (10,457,331) ikifuatiwa na Mwanza 3,834,147, Arusha 3,672,006, Mbeya 3,349,878 na Dodoma 3,111,265.

Kwa upande wa huduma za intaneti kuna ongezeko la 17% ambapo mwaka 2018 kulikuwa na Watumiaji milioni 23.8 na December 2022 Watumiaji wameongezeka hadi milioni 31.2.
 
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mohamed Moyo ameongoza zoezi la ufungaji visukuma mawimbi ‘GPS Satellite’. Collars" kwa makundi ya Tembo wanaosumbua wananchi katika Vijiji vya Wilaya za Nachingwea, Liwale na Tunduru.

Zoezi hilo linaloendeshwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), kwa kushirikiana na viongozi wa Wilaya na vijiji lilianza kutekelezwa Februari 10, 2023.

Lengo ni kusaidia kupata taarifa za wakati kuhusu mienendo na mahali yalipo makundi ya tembo na hivyo kurahisisha ufuatiliaji na kuzuia wanyamapori hao wasilete madhara kwa watu, makazi na mashamba yao.

 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita amewatoa hofu wananchi kutokana na taarifa ya kuwepo kwa ajali ya ndege akisema yalikuwa ni majaribio kwa ajili ya kupima utayari wa kuokoa katika matukio kama hayo yanapotokea.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 13 wilayani hapa, DC Mhita amesema jaribio hilo limeratibiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na kwamba hufanyika kila baada ya miaka miwili na leo ilikuwa ni zamu yakiwanja cha ndege cha Kahama.

Mbali na utayari katika viwanja vya ndege, wananchi wameshauri kuwa utaratibu wa kufanya mazoezi ya utayari uwekwe wazi ili kuepusha taharuki na madhara mengine yanayoweza kutokea.
 
Imeelezwa kuwa miongoni mwa sababu za kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa kingono kwa wavulana nchini hapa ni tabia za kuwapa vijana wanawake makahaba ili kutimiza sharti la kimila waonekane wametakaswa.

Hayo yameelezwa na Naibu Kamishna wa Thika nchini Kenya, Mbogo Mathioya wakati wa kufungua kituo kipya cha kuhifadhi wasichana na wavulana waliokutana masaibu hayo eneo la Section 9 mjini Thika Februari 11, 2023.

Mathioya amesema vijana wanaotoka jandoni wamejikuta kwenye mtego wa unyanyasaji wa kingono baada ya kufanyiwa tohara.

“Tumegundua ya kwamba wavulana baada ya kutoka jandoni hutafutiwa makahaba ili kufanya nao ngono kwa kile kinachoelezwa ni kutakaswa ili wajihisi wakamilifu kwa kuondoa maovu mwilini,” amefafanua Mathioya.
 
Mwanamume mmoja ameokolewa kutoka kwenye vifusi karibu wiki moja baada ya tetemeko la ardhi la Jumatatu kusini mwa Uturuki na Syria.

Kwa mujibu wa BBC, Huseyin Seferoglu (23) alikuwa amenasa chini ya kifusi kwa siku sita na nusu, katika jiji la Antakya.

Seferoglu ameokolewa na vikosi vya uokoaji nchini Uturuki na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

Waokoaji wameendelea kuokoa manusura zaidi kutoka kwenye vifusi nchini Uturuki na Syria huku idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea wiki iliyopita ikifikia 34,000.
 
Liverpool ameamkia kwenye derby, Salah ameamkia kwenye derby, Gakpo ameamkia kwenye derby na Darwin Nunez ameuwasha kwenye derby.
 
Tangu Lionel Messi aondoke Barcelona mauzo ya jezi namba 10 yameshuka ikiwa kwasasa anaivaa Ansu Fati, imefikia muda Barca wanachapisha jezi hiyo kwa oda maalum na kwasasa haipo kwenye maduka yao rasmi huko Catalunya, Fati amekuwa na kipindi kigumu ambapo imepeleka kuporomoka kwa mauzo ya jezi hiyo.
 
Wamiliki wa Chelsea wana imaan na Kocha wao Graham Potter, wamiliki wa Liverpool wana imaan na Kocha wao Jurgen Klopp na wote 100% wapo nyuma yao.

Chelsea na Liverpool mnasemaje?
 
“Sasa hivi akili zetu zote ni kuelekea Februari 18, siku ya vita kubwa dhidi ya Raja Casablanca na sisi tunasema moto ni uleule kwa Mkapa hatoki mtu.”

“Kama ambavyo Raja Casablanca na Horoya wamepata matokeo kwao, vivo hivyo Mnyama Simba atapata matokeo kwenye ardhi ya nyumbani.”

“Kama ambavyo walikufa wengine akina AS Vita, Al Ahly, Al Hilal, ndivyo ambavyo Raja Casablanca watakufa. Mambo ya kujadiliana tena kuhusu Horoya hayatatusaidia.”

“Ni lazima Raja Casablanca apitie moto uleule apitie mateso yaleyale waliyopitia wenzake.”

- Ahmed Ally, Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba.
 
Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji amesema kupoteza kwao dhidi ya US Monastir kwa mabao 2-0 hakujawaondolea malengo yao ya kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Arafat amesema matokeo hayo wanayapokea kama njia ya kujipanga kwa uimara zaidi kabla ya kukutana na TP Mazembe Jumapili Februari 19 nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa.

"Uzuri wa hizi mechi sio kama zile za mtoano, hapa unatakiwa kujipanga utachukuwaje pointi zako kwa ujumla wake ndani ya mechi sita utakazocheza ambazo tatu zipo nyumbani na tatu ugenini," amesema Arafat.
 
SIMBA KUTUA LEO MAPEMA
.
Kikosi cha Simba kimeanza safari ya kurejea nyumbani kutoka nchini Guinea, watapitia nchini Ethiopia na wanatarajia kuwasili Dar es Salaam leo Jumanne saa 3 asubuhi.
 
YANGA KUTUA LEO MCHANA
.
Kikosi cha Yanga kitaondoka Tunisia mchana wa leo na kutua Dubai saa 5usiku, msafara utalala hapo na leo asubuhi wataanza safari ya kurejea nyumbani ambapo wanatarajia kufika saa 8 mchana.
 
Timu 10 zilizoonyesha Kiwango Bora katika Kombe la Shirikisho Afrika raundi ya kwanza hatua ya Makundi.

NB: Yanga nafasi ya 12, pitia full list kwenye insta story

 
Habari wana JF

Habari,
Matumaini yangu wote mko poa kabisa.

Uzi huu ni kwaajili ya wote. Lengo ni kujadili changamoto zinazotukabili, pia Kupeana support katika mambo yetu hapa JF. Tupeane mbinu za kukabiliana na mambo yote hum

Karibu sana
Changamoto ni kukosa pesa ya ku hire room tumeishia vichakani
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…