Farhan Jr
Sina elimu kubwa na sayansi ya nyota kama Marehemu Sheikh Yahya, sina uwezo wa kuiona kesho hata nikipanda Mlima Kilimanjaro ila nina uhakika kabisa hata Ali Kamwe anatamani kuchambua kuhusu Clatous Chama, hata Priva anatamani kuandika kitu kuhusu Mwamba wa Lusaka na hata Alwataan anatamani ashike kipaza ahoji watu kuhusu Maestro CCC.
Amini nakwambia hata Nabi anatamani hii miguu ya Ndola huko Zambia, hata Tajiri Bakhresa anafahamu hilo ila ni ngumu kwa Msimbazi kuiachia hii dhahabu kwakuwa Mama yake hana mtoto mwingine huko Zambia.
Niamini Mimi kuna vitu ni zaidi ya Ushabiki wetu basi ni mpira wa miguu, mchezo ambao hauna mipaka na kabila, ni simulizi ya Kiungo bora zaidi kuwahi kumshuhudia kwa miaka ya hivi karibuni, sio Simba wala Yanga kila mtu anaenjoy iwe kwa kuonesha au kimoyo moyo.
That Man, is called Clatous Chama