URENO WANATINGA 16 BORA
.
FT: PORTUGAL 2-0 URUGUAY
54’—️ Bruno Fernandes
90’—️ Bruno Fernades (pen)
.
MSIMAMO KUNDI H
1. Portugal — 6
2. Ghana — 3
3. South Korea — 1
4. Uruguay — 1
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Cyprian Luhemeja, amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia ujenzi wa mtambo mpya wa maji Rufiji ambapo kwa sasa Mhandisi mshauri yupo 'site' anafanya usanifu wa mradi huo.
"Mradi huo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 750 kwa siku, ambazo zitamaliza adha ya uhaba wa maji kwa Jiji la Dar es Salaam”
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dares Salaam (DAWASA), Cyprian Luhemeja ametangaza upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaam kurejea kwa asilimia 100.
"Kwa sasa hali ya maji ni nzuri na huduma ya maji imerudi kawaida na safari hi tumerudi kwa kishindo kwani tumeongeza mtaji wa maji lita milioni 70 kutoka kwenye visima vya Kigamboni”
Tanzania ni Nchi pekee Afrika ambayo imetoa uraia kwa Wakimbizi 162,000 wa Burundi, 30,000 wa Rwanda na 10,000 wa Somali Bantus.
Mwakilishi wa Shirika la Wakimbizi Duniani upande wa Tanzania, Mahoua Parums ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa Ushirikiano kwenye masuala ya Wakimbizi katika kikao cha ndani alipokutana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu Geneva Balozi Hoyce Temu katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje.
Ikumbukwe kuwa Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Geneva inasimamia mashirika mengi ya Kimataifa ikiwemo UNHCR, Tanzania hadi leo hii inahifadhi Wakimbizi zaidi ya 260,000 mkoani Kigoma.
Kiungo kama huyu ndie anayekosekana pale Brazil kwangu na Mchezaji kama huyu ndie anahitajika kwenye kila timu, ile penati kamlazimisha Refa mpaka akatazame kwenye VAR, safi sana.
Bruno ana mtihani mkubwa sana kutoka media za England kuhusu Captain wake Ronaldo ila yeye amekuwa akitoa majibu sahihi na mazuri sana, anawanyima sana Waandishi headlines.
Pure talent, joy to watch! Anafaa kabisa kuja timu kubwa kama Chelsea.
Sina elimu kubwa na sayansi ya nyota kama Marehemu Sheikh Yahya, sina uwezo wa kuiona kesho hata nikipanda Mlima Kilimanjaro ila nina uhakika kabisa hata Ali Kamwe anatamani kuchambua kuhusu Clatous Chama, hata Priva anatamani kuandika kitu kuhusu Mwamba wa Lusaka na hata Alwataan anatamani ashike kipaza ahoji watu kuhusu Maestro CCC.
Amini nakwambia hata Nabi anatamani hii miguu ya Ndola huko Zambia, hata Tajiri Bakhresa anafahamu hilo ila ni ngumu kwa Msimbazi kuiachia hii dhahabu kwakuwa Mama yake hana mtoto mwingine huko Zambia.
Niamini Mimi kuna vitu ni zaidi ya Ushabiki wetu basi ni mpira wa miguu, mchezo ambao hauna mipaka na kabila, ni simulizi ya Kiungo bora zaidi kuwahi kumshuhudia kwa miaka ya hivi karibuni, sio Simba wala Yanga kila mtu anaenjoy iwe kwa kuonesha au kimoyo moyo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.