

Farhan Jr
Yupo hapo Mkurugenzi wa bodi ya ubashiri Tanzania (The gaming board of Tanzania) kamwe hawezi kushiriki kwenye kitu ambacho sio cha kweli
Yupo hapo mtu kutoka Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambao wao kisheria wanachukua 25% ya mapato ya Sports Betting, hawezi kushiriki kwenye kitu ambacho sio cha kweli
Guys hii nchi ina mifumo yake, Simba hawezi kuja kutangaza mkataba wa uongo mbele ya serikali, kamwe Simba hawawezi kusema uongo wa aina hiyo ya kuchezea NAMBA ambazo ni mapato
Huu mkataba Simba wameupata sio kwa bahati mbaya ni kutokana na kazi waliyoifanya kwa miaka minne nyuma, nani ambaye haitaki traffic ya Simba mtandaoni? Nani hataki kujihusisha na fan base ya Simba?
Trust me! Simba wanavuna leo walichokipanda miaka minne nyuma, baada ya MO Dewji kuweka pesa iliyozaa mfumo, mfumo uliozaa weledi, weledi ulioleta mafanikio ndicho kinachowalipa sasa
NI BILLION 26.18 NA IMETHIBITISHWA NA MAMLAKA, MIE NANI NIPINGE? TUISHI NAYO HII TAARIFA! GUYS HAKUNA KITU KINAFANYIKA BILA MACHO YA MAMLAKA, HAKUNA
Usikasirike ni mchakato ambao ulichukua muda, watu wakatumia muda na sasa wanavuna matunda ya muda! Beba makombe, nenda Afrika washa moto basi hizi noti zipo tu