[emoji3578] Shaffih Dauda
Mara kadhaa nikipata wasaa wa kuzungumza na vijana wangu au mtu yoyote mwenye ndoto huwa napenda kumsikiliza zaidi yeye, nijue kama anajiamini kwenye chochote anachokipigania.
Kama jibu ni NDIO basi ni rahisi kuisukuma ndoto hii na kuifanya iishi, cha kwanza lazima moyo wako uwe tayari kisha acha kila kitu na wekeza kwenye hiyo ndoto, amka sali sana, pakikucha kapambane sana.
Hakuna uchawi wowote, believe me there is no magic kwenye mafanikio, ni matokeo tu ya kutoka kwenye dimba la kubweteka na kusimama kila leo ili kuwa mpya.
This is my very humble advise kwa yoyote mwenye ndoto, nawaamini sana wale wanaoota ndoto na kutaka kuiishi, kwa nafasi yako, kwa nguvu zako kwa ajili ya kesho yako.
Hakuna jipya duniani, hakuna siri ya mafanikio zaidi ya kufanya ambacho moyo hautaki tena kwa kujilazimisha, ushindi upo hapo.
NDOTO, NDOTO, NDOTO amka kaiishi ndoto
DiGALA