Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220723-073516_Opera%20Mini.jpg
 
Mwanaume mmoja Raia wa Marekani Bradley Robert Dawson anashikiliwa na Polisi kwa kumuua mkewe walipokuwa kwenye honeymoon (fungate) kwenye hoteli ya kifahari huko visiwani Fiji.

Jeshi la Polisi katika eneo hilo limethibitisha kuwa alasiri ya Julai 9, mwanamke aliyetambuliwa kuwa ni raia wa Marekani Christe Chen mwenye umri wa miaka 36 alipatikana akiwa amefariki kwenye sakafu ya chumba chake katika visiwa vya Yasawa huko Fiji.

Wafanyakazi wa Hoteli hiyo waliwaambia Polisi kwamba Chen amefariki baada ya kupigwa na mume wake wakiwa fungate katika eneo hilo.

Mume wa Chen, aliyetambuliwa kama raia wa Marekani Bradley Robert Dawson mwenye umri wa miaka 38, alipatikana na kukamatwa siku mbili baadaye huko Nadi, mji ulioko kwenye pwani ya magharibi ya kisiwa kikuu cha Fiji, Viti Levu.
Screenshot_20220723-074901_OGInsta%2B.jpg
 
Mwili wa Dereva Bodaboda Dominick Kigula (31) aliyeuwawa kwa kuchomwa kisu yeye pamoja na Mpenzi wake Esther Shiyago (25) amezikwa leo Julai 22, 2022 katika makaburi ya Sechelela yaliyopo kata ya Makulu Dodoma.

Wawili hao waliuawa alfajiri ya Jumatano wakiwa kwenye nyumba aliyopanga Dominick mtaa wa Msangalee, kata ya Dodoma Makulu jijini Dodoma na hadi sasa Mtuhumiwa wa mauaji haya hajatajwa na Polisi lakini inaaminika kuwa chanzo ni wivu wa kimapenzi.

Marehemu Dominick ameacha mtoto wa miaka minne.
Screenshot_20220723-075004_OGInsta%2B.jpg
 
Hatimaye Urusi imekubali nafaka ya Ukraine ianze kuuzwa nje ya Nchi hiyo, hii ni kutokana na mkataba uliosainiwa huko Istanbul, Uturuki na kuhusisha pande zote ikiwemo Urusi.

Wajumbe wametia saini makubaliano ambayo yataruhusu karibu tani milioni 20 za nafaka ambazo zimekuwa zikizuiliwa na Urusi, kusafirishwa kutoka Ukraine kwenda kwenye Nchi mbalimbali kama ilivyokuwa ikifanyika kabla ya vita.

Mkataba huo uliotiwa saini na Urusi, Ukraine, Umoja wa Mataifa na Uturuki umetajwa kuwa ni msingi wa matumaini ambapo Uturuki imesema itakuwa ikikagua meli zote kuhakikisha kuwa hazibebi silaha.

Mkataba huu kusainiwa imechukuliwa kama ushindi wa kidiplomasia katika vita hiyo kati ya Urusi na Ukraine ambavyo sasa inaingia mwezi wa sita.
Screenshot_20220723-075116_OGInsta%2B.jpg
 
Majambazi sita wamejeruhiwa kwa risasi na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM usiku wa kuamkia leo katika Barabara ya Mbozi iliyoko Keko Wilaya ya Temeke.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne amesema kundi la majambazi wapatao tisa wakiwa na silaha moja aina ya pistol, mapanga manne na funguo nyingi za kutendea uhalifu, waliwatishia maisha walinzi kwa silaha na kuwafunga kamba, baadaye wakaingiza gari aina ya Hiace kwenye godown ili kuiba spare za magari”

“Polisi walipopata taarifa walifika haraka eneo la tukio na wakalikuta kundi hilo na wakaanza kuwatishia Askari kwa silaha, Polisi nao wakajihami”

“Majambazi sita wamejeruhiwa na wamekimbizwa Hospitali kwa ajili ya matibabu ili tuweze kupata fursa ya kuwahoji kwa kina, wengine tupo nao na uchunguzi wa tukio hili unaendelea, zaidi ya boksi 70 zilitaka kuibiwa”
Screenshot_20220723-075247_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dr Damas Ndumbaro amesema kuwa Wiki mbili zilizopita Mtu mmoja alikamatwa nchini Poland akiwa na kobe zaidi ya 100 wakitokea nchini Tanzania bila ya kuwa na vibali vya usafirishaji .

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kikosi kazi cha ulinzi kwa Watoto dhidi ya biashara ya usafirishaji haramu wa Binadamu ambacho kinaundwa na Maofisa wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama na kuwataka katika majukumu yao waongeze pia kudhibiti wa usafirishaji wa rasilimali za nchi kwa maana inaonekana kuna uzembe ulifanyika hapa Tanzania Airport kwa mtambo wa kuscan kutokufanya kazi ipasavyo.
Screenshot_20220723-075339_OGInsta%2B.jpg
 
Majambazi sita wamejeruhiwa kwa risasi na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM usiku wa kuamkia leo katika Barabara ya Mbozi iliyoko Keko Wilaya ya Temeke.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne amesema kundi la majambazi wapatao tisa wakiwa na silaha moja aina ya pistol, mapanga manne na funguo nyingi za kutendea uhalifu, waliwatishia maisha walinzi kwa silaha na kuwafunga kamba, baadaye wakaingiza gari aina ya Hiace kwenye godown ili kuiba spare za magari”

“Polisi walipopata taarifa walifika haraka eneo la tukio na wakalikuta kundi hilo na wakaanza kuwatishia Askari kwa silaha, Polisi nao wakajihami”

“Majambazi sita wamejeruhiwa na wamekimbizwa Hospitali kwa ajili ya matibabu ili tuweze kupata fursa ya kuwahoji kwa kina, wengine tupo nao na uchunguzi wa tukio hili unaendelea, zaidi ya boksi 70 zilitaka kuibiwa”View attachment 2300715
Duh
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

Wakiuliza ni nani pembeni yake, waambie ni Augustin Azuka, wakiuliza ni nani waambie ni JAY JAY OKOCHA, ndio alikuwa fundi sana mpaka akapewa jina mara mbili

Wakiuliza ilikuwaje huyo mtoto pembeni akasimama nae? Kwanza waambie anaitwa Pape “THE PAPA OF STUNNERS”Ousmane Sakho kutoka Senegal [emoji1211] ambaye alicheza Simba

Wajukuu watauliza ilikuwaje sasa akawa hapo? Waambie ulikuwa ni mwaka mmoja ambao alipiga goli bora sana pale Taifa dhidi ya Asec Mimosa ya Aziz Ki, kwenye michuano mikubwa Afrika na sio kombe la Kuku pale Ketaketa huko Ulanga, Morogoro

Watauliza ulikuwa mwaka gani Babu? Ee bhna wewe futa kwanza machozi kisha waambie, ni mwaka ambao baridi ilikuwa kali sana Dar Es Salaam, mwaka ambao mpaka Kariakoo walivaa masweta, naam ndio mwaka huo

Kwani hilo bao lilikuwaje Babu? Futa tena machozi kisha waambie, ilikuwa krosi hatari sana ya Mjukuu wa Mbaraka Mwinshehe, ilikuwa krosi ya Mluguru wa Morogoro @shomari_12_kapombe moja kati ya beki bora kizazi kile

Babu mbona unalia sana? Wajukuu zangu nalia kwakuwa naumia, nadhani japo sina uhakika niliishi kuishuhudia Simba bora zaidi kuwahi kutokea ambayo hamtopata bahati ya kuiona kwakuwa its once in a lifetime

Pole sana Babu tunakuhurumia sana! Hapana Wajukuu zangu jihurumieni ninyi ambao hamkupata kuishi kuliona bao hilo, hamkupata kuishi kumfahamu hata Clatous Chama kutoka Zambia, au Aishi Manula wa Morogoro

Nawahurumieni ninyi na vizazi vyenu kwakuwa hamkuwahi kupata kuiona Simba bora kuwahi kutokea, endeleeni kuenjoy na simulizi za @gharib_mzinga23 @mwakalobo_jr pale Youtube ya AZAM TV, lakini sisi tuliishi kuyaona

Mzinga yupo zake Kilwa hivi sasa kazeeka, yule Mwakalobo karudi zake Mbeya anakula pombe na Wanyakyusa wenzake, ziko wapi zile nyakati??

View attachment 2300664
hahahahaha,uko vzr ktk uandishi
 
.....dalili zinaonesha kazi nimepata mdau. Mimi nalinda kwa zana za jadi, na siku hizi nimeadvance kiasi, si unajua mambo ya tekno-lojia kwenye lindo natumia zana za jadi na kienyeji.
Barua nakuandikia kwa SLP ngapi?
Hahaha hahaha hapa tayari kazi umepata tatizo nakumbuka uliniuzia korosho ulizo changanya na kokoto nikiwaza tu hivyo nguvu zinaniishia
 
Back
Top Bottom