[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
Wakiuliza ni nani pembeni yake, waambie ni Augustin Azuka, wakiuliza ni nani waambie ni JAY JAY OKOCHA, ndio alikuwa fundi sana mpaka akapewa jina mara mbili
Wakiuliza ilikuwaje huyo mtoto pembeni akasimama nae? Kwanza waambie anaitwa Pape “THE PAPA OF STUNNERS”Ousmane Sakho kutoka Senegal [emoji1211] ambaye alicheza Simba
Wajukuu watauliza ilikuwaje sasa akawa hapo? Waambie ulikuwa ni mwaka mmoja ambao alipiga goli bora sana pale Taifa dhidi ya Asec Mimosa ya Aziz Ki, kwenye michuano mikubwa Afrika na sio kombe la Kuku pale Ketaketa huko Ulanga, Morogoro
Watauliza ulikuwa mwaka gani Babu? Ee bhna wewe futa kwanza machozi kisha waambie, ni mwaka ambao baridi ilikuwa kali sana Dar Es Salaam, mwaka ambao mpaka Kariakoo walivaa masweta, naam ndio mwaka huo
Kwani hilo bao lilikuwaje Babu? Futa tena machozi kisha waambie, ilikuwa krosi hatari sana ya Mjukuu wa Mbaraka Mwinshehe, ilikuwa krosi ya Mluguru wa Morogoro @shomari_12_kapombe moja kati ya beki bora kizazi kile
Babu mbona unalia sana? Wajukuu zangu nalia kwakuwa naumia, nadhani japo sina uhakika niliishi kuishuhudia Simba bora zaidi kuwahi kutokea ambayo hamtopata bahati ya kuiona kwakuwa its once in a lifetime
Pole sana Babu tunakuhurumia sana! Hapana Wajukuu zangu jihurumieni ninyi ambao hamkupata kuishi kuliona bao hilo, hamkupata kuishi kumfahamu hata Clatous Chama kutoka Zambia, au Aishi Manula wa Morogoro
Nawahurumieni ninyi na vizazi vyenu kwakuwa hamkuwahi kupata kuiona Simba bora kuwahi kutokea, endeleeni kuenjoy na simulizi za @gharib_mzinga23 @mwakalobo_jr pale Youtube ya AZAM TV, lakini sisi tuliishi kuyaona
Mzinga yupo zake Kilwa hivi sasa kazeeka, yule Mwakalobo karudi zake Mbeya anakula pombe na Wanyakyusa wenzake, ziko wapi zile nyakati??