[emoji3578] Farhan Jr
Mwalimu wangu aliwahi kuniambia katika michezo yote duniani, basi ni mpira wa miguu ambao umebeba MTAA na MAISHA yetu ya kawaida
Mwalimu aliniambia mpira wa miguu ni mtaa ambao umewekewa mfumo tu, lakini ili mpira wenyewe uwe na mvuto basi unauhitaji mtaa kwenye mpira
Mwalimu aliniambia China wamewekeza sana ila mpira hauna mvuto licha ya kuwa asili yake ni China ila mitaa haiushi mpira kuanzia Beijing, Shanghai hadi Hong Kong, hii ipo mpaka Marekani pia
Kwakuwa mpira ni mtaa, wangapi wamewahi kuwajibu vibaya wazazi wao kwasababu ya mpira?, wangapi wamekosana na mpaka kununiana kisa mpira? Wangapi wamepigana kisa mpira?
Najua ni wengi, basi hii ni kwakuwa mpira ni MTAA na ndio MAISHA yetu halisi! Chochote kinachotokea banda umiza au uwanjani hawi Binadamu wa kawaida unaemfahamu bali kila Mtu kwenye dunia yake
Mungu akinijalia umri mrefu, Mwanangu RIYAD hata kama atanitolea lugha chafu kisa mimi Simba na yeye Yanga basi sitompa adhabu, hata Mke wangu akinimind kisa mimi Chelsea yeye Man United sitomind kwakuwa ni MAISHA halisi
Kwakuwa mpira ni Mtaa uliopewa MFUMO, basi Nikutakie mapumziko mema Kaka @hajismanara bahati mbaya tu uliuishi mtaa kwenye Mfumo, lakini pongezi kwa @tanfootball kwa kusimamia sheria kadri inavyotakiwa
Leo amefungiwa moja ya icon ya mpira wetu, aliyeuishi utamaduni halisi wa mpira kwenye dunia ya mfumo, haikuwa rahisi ila alileta kitu chake kwenye game!
Farhan ni mtafutaji wa kawaida tu kutoka Morogoro ambaye hapendi kuona watafutaji wengine wanapatwa na kadhia, kama nilivyosimama na Kocha Mbwana Makata basi hata kwa Haji pia, MUNGU AWABARIKI[emoji1488]