[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
Wakati nasoma course ya Sports Management nakumbuka Mwalimu aligusia kitu kuhusu FOOTBALL FANS EVOLUTION, namna Mashabiki wanabadilika kutoka kizazi hadi kizazi
Alisema βIn every generation there will be fans with distinctive characters than the former and the latter, very sad but lets agree, football is loosing its true custodiansβ akamaliza
Ndio zamani Wazee wetu waliweza kushabikia timu zao, wakamuimba Sunday Manara au Zamoyoni Mogella ingali hata machoni hajawahi kumuona, akaisifia Reli, Pamba, Simba, Tukuyu Stars au Yanga ingali hajawahi kuiona, walikuwa Mashabiki halisi
Kikaja kizazi kingine na sifa zake za kipekee, sasa tupo kwenye kizazi cha mpira cha mizuka, umaarufu na tambo nyingi sana ambazo zinaathiri moja kwa moja wachezaji na timu zetu
Leo hii itaundwa hoja ya kumkataa Gael Bigirimana hata kama profile yake ipo wazi, leo hii watamkataa Kapama hata kama anaweza kuleta kitu, wananuna kwakuwa wapo kwenye kizazi cha Showbiz na window shopping
Tupo kwenye kizazi cha mpira ambacho kinataka tuendeshe Bugatti inayotumia injini ya Bodaboda, tupo kwenye kizazi kinachotaka uongo mtamu kuliko ukweli mchungu
Viongozi na Benchi la Ufundi wawe makini na hiki kizazi chetu, wasifanye vitu kisa watu watasemaje! Wafanye kulingana na mahitaji ya timu
Tupo kwenye kizazi hiki ambacho Mchizi yupo na Manzi geto wanacheck season za Kikorea wakati Nassor Kapama anazima pale Kagera, hajawahi kumuona
Tupo kwenye kizazi ambacho Mchizi yupo photoshoot wakati Habib Kyombo anakichafua pale Majimaji, hajawahi kutazama mechi ya Mbeya Kwanza ila ataponda usajili
Tupo kwenye ambacho Gael Bigirimana anaupiga pale EPL ila Msela huku yupo busy kukata pindi Mchikichini ila ataponda usajili