[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
Huyu ni Kiungo Said Khamis Ndemla, naomba niwape kisa kimoja kuhusu Kiungo huyu na Mtibwa Sugar
Ndemla yupo Manungu kwa mkopo akitokea Simba ambapo anamalizia mkataba wake sasa na tayari amejiunga na Singida Big Stars
Ikumbukwe Ndemla alipata kadi nyekundu dhidi ya Simba na alikosa mechi mbili, dhidi ya Namungo na Yanga, lakini ngoja niwape kisa kimoja
Baada ya mechi Ndemla aliwasha gari yake binafsi na kuanza safari ya kuelekea Manungu akitokea nyumbani kwake Kigamboni, licha ya kuwa hayupo sehemu ya mchezo dhidi ya Namungo aliwaambia anaenda kuwasupport wenzake, IMAGINE
Kutokana na umbali mrefu aliingia Manungu usiku sana na kweli siku ya mechi alikuwepo uwanjani na aliwapa support wenzake japo Mtibwa alifungwa, akarejea tena Dar Es Salaam kwa usafiri wake binafsi, IMAGINE
Siku ya mechi ya Yanga alifika tena uwanjani kuwapa support wenzake na Mtibwa alipoteza tena ile mechi, rasmi Mtibwa ikaenda Playoffs dhidi ya Prisons! Timu ikitakiwa kusafiri usiku ule kuelekea Mbeya
Kumbuka Ndemla hapo amemaliza adhabu ya mechi mbili lakini hata mkataba wake wa mkopo pale Mtibwa sasa unamruhusu kutoitumikia tena timu akihitaji au akiwaambia tu kuwa hayupo tayari au angeongopa anaumwa, ila kwake ilikuwa tofauti
Alipiga simu kwa Mkewe alete baadhi ya nguo zake na viatu vyake kwenye hotel ya timu pale Kijichi na kumwambia anaelekea Mbeya na timu, wanaenda kupambana pamoja na Ndugu ili timu isalie, hakutaka kukimbia vita na kuwaacha Ndugu zake, IMAGINE! Saa tatu usiku timu iliondoka Dar kuelekea Mbeya, Ndemla akiwemo pia
Kwenye mechi ambayo Ndemla alipiga mpira mkubwa sana akihusika kwenye mabao takribani mawili na timu ilikuwa na balance sana, alitutumikia kwa wema sana Wana Morogoro
Nilimuuliza Ndemla kwanini una moyo kama huu? Kwanza ni heshima yake kwa Mtibwa, wachezaji wenzake na CEO @swabr04 ambaye anaishi nao kwa wema sana, CEO hana baya na mtu, hivyo anajiona ni sehemu ya familia na ana deni la kuibakiza timu
@mtibwaofficial inakuheshimu, MOROGORO inasema Asante, MANUNGU itakuaga kwa heshima kwenye mchezo wako wa mwisho kwenye jezi yetu pale Manungu dhidi ya Prisons