Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Vijana wa Jamii ya wafugaji wa kabila la Wasukuma kuwalazimisha Wanawake Kwa nguvu kufanya nao mapenzi na kutaka kuwaoa bila ridhaa yao, DC Ngollo amesema mila hizo maarufu kwa jina la Chagulaga zimepitwa na wakati.

Kauli hiyo ameitoa akiwa katika Kijiji Cha Igumbiro katika mwendelezo wa ziara yake ya kusikiliza kero za Wananchi katika Vijiji vya Wilaya hiyo, jambo hilo liliibuka baada ya Wanawake kutoa malalamiko yao Kwa DC @ngollomidalla akiwa Kijijini hapo na kusema kuna baadhi ya Wanaume wanalazimisha Wanawake kufanya nao mapenzi ama kuwaoa bila ridhaa yao na hufanya hivyo kwa kuwavizia Wanawake wakiwa wanaenda shambani au wakiwa kwenye minada.

Wananchi wanasema Wanaume hao wakikutana na Wanawake humzunguka na kumwambia achague Mtu mmoja afanye nae mapenzi na akikataa analazimishwa “Mwanamke akikataa anapigwa viboko kama kuna Baba yako au Bwana wako akija anapigwa viboko na yeye"

DC Ngollo amekemea tabia hiyo na kusema huo ni ubakaji na Serikali haitafumbia macho Mtu au kikundi chochote cha Watu wenye tabia hiyo “"Suala la Chagulaga lilikuwa enzi za Mabababu zetu, ni ubakaji kama umempenda Mwanamke si uende ukazungumze nae, usione soo sema nae sasa unaenda kuvamia inaonesha mdomo wako ni mzito huna ujasiri wa kwenda kumtongoza Mwanamke, domo zege, tutakuja na Kampeni ya kupinga vitendo hivi”
Screenshot_20220707-041902_OGInsta%2B.jpg
 
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa iliyokaa kikao chake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Njombe imewahukumu Washtakiwa watatu Elias Jackson Mwenda (31), Hussein Khamis (31) na Orestus Mbawala (51) kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya James Kaengesa mkazi wa Makambako mkoani Njombe.

Akisoma hukumu hiyo jaji Dk.John Utamwa amesema tukio hilo la mauaji lilitokea mtaa wa Mashujaa uliopo halmashauri ya mji wa Makambako hapa mkoani Njombe.

Amesema tukio hilo lilitokea Juni 2016 majira ya saa mbili usiku ambapo marehemu ambaye alikuwa dereva wa bodaboda aliyokuwa akiimiliki alikodiwa na moja ya washtakiwa hao na alipofika eneo la Mashujaa aliambiwa asimame na mshtakiwa huyo ambaye alikuwa amepakiwa kwenye bodaboda hiyo.

"Aliposimama ndipo walimkaba marehemu na kumnyonga kwa kutumia kamba ambayo waliitengeneza mkoani Njombe na kupora pikipiki"

Baada ya kumyonga marehemu na kumuua amesema washtakiwa hao walimtupa kwenye shamba la mahindi na kutoweka na pikipiki kuelekea mkoani Mbeya ambapo walikamatwa eneo la Rujewa wakiwa na pikipiki hiyo.
Screenshot_20220707-042009_OGInsta%2B.jpg
 
Mbunge wa Pangani, Jumaa Aweso mapema leo Jumatano Julai 6, 2022 amefanya ziara na kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Tanga-Pangani.

Akiwa kijiji cha Choba Aweso ambaye pia ni Waziri wa Maji amezungumza na wananchi wa eneo hilo na kuwasihi kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita kwani inayo dhamira ya dhati ya kukumilisha Mradi huu kwa wakati.
Screenshot_20220707-042646_OGInsta%2B.jpg
 
Watumishi wawili wa kitengo cha ardhi katika Jiji la Dodoma wamefukuzwa kazi na wengine watano wamesimamishwa kwa kusababisha migogoro ya ardhi.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano, Julai 6, 2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa jiji Joseph Mafuru katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Mkoa kilipokutana na watumishi wapya wa idara ya ardhi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho kilichokuwa kikijadili mikakati ya kumaliza migogoro ambayo imetajwa kukita mizizi na kulifanya jiji hilo liongoze kwa migogoro.

Katika kikao hicho, Mafuru amesema sababu iliyowaingiza matatizoni watumishi hao ni uuzaji na viwanja na kubadili matumizi ya maeneo kwa lengo la kujipatia kipato.

“Mfano mzuri ni eneo lile la Mwanga Bar, tangu 1978 ni eneo wazi lakini mtu ghafla kaibuka na kubadili matumizi yake eti akapima viwanja na watu wakaanza kujenga, hilo ni tatizo,” amesema Mafuru.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema hatawavumilia watumishi wanaosababisha migogoro ya mara kwa mara kwakuwa wanawafanya watumishi wengine washindwe kuwahudumia wananchi na kutumia muda mwingi zaidi kutatua au kuendesha mazungumzo ya migogoro.
Screenshot_20220707-042741_OGInsta%2B.jpg
 
LUIS ANARUDI SIMBA [emoji837]
.
Hadi Kufikia leo jioni tayari 90% ya dili la Luis Miquissone [emoji1174] kutoka Al Ahly [emoji1093] kurejea Simba [emoji1241] linaelekea kutimia.
.
[emoji187]: “Miquissone anaipenda Simba, ameomba arejee kwenye kikosi, maana amekumbuka lile ‘vaibu’ na upendo ambao alikuwa anapewa na mashabiki wake, pia familia yake inataka aishi Tanzania. Wakati wanaongea sana, sisi tutafanya kwa vitendo, nadhani muda utafika mashabiki wetu wataanza kupata raha.” Kimesema chanzo changu makini ndani ya Simba.
Screenshot_20220707-043142_OGInsta%2B.jpg
 
ZORAN MAKI NA FALSAFA MPYA
.
Kocha mpya wa Simba, Zoran Maki mwenye leseni ya UEFA A Pro anapendelea sana soka la kujilinda na kushambulia kwa kasi huku akipendelea kutukia mifumo ya 4-4-2, 5-3-2 na 4,3,3 katika mechi zake nyingi.
.
Huenda Simba ikabadilika kiuchezaji kutoka kwenye soka la pasi fupi fupi na kwenda kwenye pasi ndefu za mbali na kuwa na kasi katika kutengeneza nafasi.
Screenshot_20220707-043301_OGInsta%2B.jpg
 
SUMA: NIMEMZIDI MGOMBEA MWENZANGU
.
[emoji860] “Nimemzidi mgombea mwenzangu, yeye Kitaaluma ni mtunza pesa mimi ni Mtafutaji wa pesa, nina uwezo wa kubuni na kuibua Miradi ya kuleta pesa, pia mhamasishaji, sasa utatunza pesa ambazo hazipo?? Hazijatafutwa?" - @sumamwaitenda

#SautiYaWananchi
Screenshot_20220707-043458_OGInsta%2B.jpg
 
YACOUBA NDO BASI TENA !!
.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya klabu ya Yanga kuna wachezaji watatu wamepewa mkono wa kwaheri.
.
Wachezaji hao, Deus Kaseke, Balama Mapinduzi na Paul Godfrey ‘Boxer’ na Yacouba Sogne atatolewa kwa mkopo.
.
Jana Jumanne, wachezaji waliitwa ofisi za mfadhili wa klabu hiyo (GSM) kwa lengo la kumalizana nao na kuwatakia maisha mema kwenye majukumu yao mapya nje ya Yanga.
Screenshot_20220707-044221_OGInsta%2B.jpg
 
Mshambuliaji Angel Di Maria amekubali kujiunga na Juventus kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya mkataba wake kumalizika PSG.

Di Maria, 34, anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Juventus bila ada ya usajili kutokana mikataba yao kumalizika baada ya awali kumalizana na Paul Pogba.
Screenshot_20220707-044340_OGInsta%2B.jpg
 
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema baada ya kupoteza makombe yote msimu huu sasa wanajipanga na msimu ujao kikosi chao kitakuwa bora zaidi kulingana na usajili bora waliofanya wakati huu wa dirisha kubwa la usajili.
Try Again alisema jambo la kwanza walichukua ripoti ya kocha wao aliyeondoka, Pablo Franco pamoja na mawazo ya baadhi ya viongozi wenye uelewa wa masuala ya kiufundi kisha wakaenda sokoni kutafuta wachezaji wa maana.

Kocha mpya wa Simba, Maki, wachezaji wapya na wale waliomaliza msimu na kikosi hicho wapo kwenye mipango ya msimu ujao wanatakiwa kuwa Dar es Salaam Julai 13 kwani kati ya Julai 14 au 15 wataondoka nchini kwenda kwenye moja ya nchi iliyokuwa na asili ya Kiarabu Afrika kwa ajili ya kambi (Pre-season). Mwanaspoti linajua Simba inaenda kambini Misri.

Nyota waliosajili lakini hawajawatangaza ni Vicent Akpan, Augustine Okra, Habibu Kyombo, Ceasar Lobi Manzoki, Nassoro Kapama na Phiri ambaye ametangazwa tayari wiki kadhaa nyuma.

Screenshot_20220707-044440_OGInsta%2B.jpg
 
Msanii Robyn Rihanna Fenty maarufu Rihanna ametajwa kwenye jarida Forbes ya 2022 kuwa ndiye bilionea wa kike mwenye umri mdogo zaidi nchini Marekani akiwa utajiri wenye thamani ya dola 1.4billion.

Rihanna⁠ ambaye ukiachana na kuwa msanii pia ni mwigizaji na mfanyabiashara akiwa kama mmiliki mwenza wa kampuni ya vipodozi ya Fenty Beauty akimiliki asilimia 30 ya hisa katika bidhaa zake za nguo za ndani ya Savage x Fenty⁠, pia ndiye bilionea wa kwanza kutoka taifa la Barbados akitajwa kama mwanamke pekee tajiri wa umri chini ya miaka 40.
Screenshot_20220707-044544_OGInsta%2B.jpg
 
Mshambuliaji anayetajwa kusajiliwa na Yanga, Stephan Aziz Ki amekoleza hatua ya kukaribia Yanga baada ya kumtakia heri mgombea wa nafasi ya urais ndani ya klabu hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ki ameweka kipeperushi cha mgombea Urais katika uchaguzi wa Yanga injinia Hersi Said huku akiandika kwa ufupi 'Kila la kheri Bosi'.

Hersi ndiye mgombea pekee wa nafasi hiyo ya urais ndani ya Yanga katika uchaguzi utakaofanyika Julai 9, 2022.
Kutokana na ujumbe huo wa KI naye Hersi amemjibu mshambuliaji huyo kupitia akaunti yake akiandika ahsante kijana wangu.
Screenshot_20220707-044640_OGInsta%2B.jpg
 
Manchester United imemsajili beki wa kushoto, Tyrell Malacia kutoka Fayenoord kwa kitika cha Euro 14.7 na mkataba wa miaka minne.

Beki huyo ataitumikia United mpaka 2026 kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Screenshot_20220707-044740_OGInsta%2B.jpg
 
RASMI | Inaki Williams amechagua kuvaa jezi ya timu ya taifa ya Ghana [emoji1110] kuelekea michuano ya kimataifa

Inaki alishawishiwa na FA ya nchi hiyo, baada ya taratibu zote rasmi nyota huyo wa Athletic Bilbao atacheza Black Stars
Screenshot_20220707-044931_OGInsta%2B.jpg
 
RASMI | Kinda Tariq Lamptey amebadili uwakilishi wake kwenye soka la kimataifa na sasa atahudumu kwenye timu ya taifa ya Ghana [emoji1110] na sio Uingereza tena
Screenshot_20220707-045022_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom