Unaenda kwa CR7 ambaye unafahamu anahitaji Mwanamke bora kwa watoto wake watatu ambao amewapata kwa Mama wawili tofauti, Georgina hakuwa na shaka
Unaenda kwa CR7 ambaye ana Dada wawili wenye gubu, ndio Mawifi fulani wa Kireno wenye Uafrika ndani yao[emoji3] Elma na Katia, inasemekana wadada wengi walishindwa kuendana nao
Lakini Binti huyu hakujali hilo alijiapiza kuwa hiyo ndio nafasi pekee ya binti kutoka Jaca, kaskazini mwa Hispania aliyekuwa na maisha magumu sana
CR7 kwao ni mtoto wa mwisho, Mama yake Maria anamtazama yeye kama kidonda, Dada zake wote na Kaka yake Hugo wote wanampenda sana, ndio maana wamekuwa wakiamua sana kuhusu nani awe na CR7
Gio hakufanya makosa, picha linaanza Cristiano Jr ni kama Mtoto wa kumzaa, tumia muda wako kaperuzi page yake picha nyingi amembeba Mateo au Eva na sio mwanae wa kumzaa Alana Martina[emoji3]
Hizo code ni hatari mno! Mama anapenda zaidi watoto ambao hajawazaa, ndio namna unawin game! Picha nyingi Ronaldo au Cristiano Jr ndio wapo na Alana (Bint yake wa kumzaa) yeye yupo na Wanae wa kufikia
Ndicho familia ya Ronaldo ilikuwa inahitaji, Mama wa familia zaidi! Bibie huyu kwasasa ndie kipenzi cha familia ya Ronaldo, wanacomment sana kwenye page yake na wamemkubali sana
Gio ana Dada yake anaitwa Ivana, wote mwendo ni ule ule, nafasi kubwa wamewapa watoto wa kufikia[emoji3] wanawapenda sana watoto wa CR7!
Ivana anampenda sana Mume wa Mdogo wake, mara nyingi amekuwa akimpost CR7, Ronaldo huwa hana tabia ya kula bata sana na watu tofauti na Ndugu zake na Masela zake ila kwa familia ya Gio imekuwa tofauti, kawapa nafasi kubwa
Hakuwahi mvalisha bint pete rasmi ya uchumba ila kwa Gio ameweza na ni wachumba rasmi!
Maisha yanataka nini tena kwa Gio?? [emoji3]