Imeandikwa na @swalehmawele
[emoji344] Inasemekana kuwa Victor Akpan amemalizana na Simba kwa ajili ya kuitumikia klabu yao msimu ujao, ngoja nikwambie kitu, Victor Akpan ni defensive midfielder ( kiungo mzuiaji ) lakini kitu cha ziada kwake ni uwezo wake wa kupiga pasi za mbele anapohitajika kufanya hivyo.
[emoji344] Twende kwa viungo waliopo Simba, Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin wote ni box to box midfielders kwa maana ya viungo wanaocheza baina ya maboksi mawili, viungo wanaocheza katika patterns zote za kulinda na kushambulia ( defensive & offensive patterns ).
[emoji344] Jonas Mkude ni holding midfielder, si mzuri sana katika kukaba 1 v 1, ni nadra sana kumuona Mkude anapiga slide tackling, yeye anaweza kuutunza mpira, kupiga pasi na kuzuia eneo ( zonal marking ), kuna utofauti wa kuzuia mtu na eneo, si kama Jonas hawezi kukaba kabisa, anaweza lakini si kama anavyofanya Thadeo au Akpan.
[emoji344] Kwanini Thadeo na Akpan, hawa wote ni defensive midfielders, wanafikiria zaidi kukaba, wanafikiria zaidi kuwalinda mabeki wa kati, utawaona kwenye matukio mengi ya kugongana kwa sababu ya aina yao ya mchezo na majukumu yao ndani ya kiwanja, kwa bahati mbaya Thadeo hajarudi katika form yake kutokana na majeraha.
[emoji344] Kama Simba wameamua kumsajili Akpan ni mchezaji mzuri ingawa bado wanahitaji kuifikiri tena nafasi hiyo, bado nawaona wakihitaji kuliongezea nguvu eneo lao la kiungo wa chini, ukiwa na viungo wawili wakabaji aina ya Akpan jumlisha na Mkude ambae anaweza kutumika kama holding hiyo ni bima kwao.
[emoji344] Msimu huu wamelazimika kumtumia Sadio kama kiungo wa chini kutokana na kukosekana kwa Mkude na Thadeo, vipi kama wangekuwa na mtu mwengine wa kuziba nafasi zao? nalisema hili kwa sababu pia sioni Simba wakiendelea kudumu na Thadeo Lwanga hiyo maana yake watakuwa na Akpan pekee ambae ana sanaa kubwa ya uzuiaji.
Nb: Tusimchukulie kwa wepesi kwa sababu Akpan anatoka Costal Union, tuangalie quality ya mchezaji, Kagere alitoka Kenya, Luis alitoka Msumbiji na wachezaji wengi walioibeba Simba wametoka katika ligi dhaifu kuliko sisi, huo ni mfano tu, usiangalie nani anatoka wapi, angalia quality.