Makapuku Forum

GREENWOOD KUPANDA KIZIMBANI
.
Kinda wa Manchester United, Mason Greenwood atapanda kizimbani kwa mara ya kwanza, kusikiliza kesi yake inayomkabili tangu alipokamatwa Januari mwaka jana.
.
Greenwood anashutumiwa kwa kesi mbili ya ubakaji na kutishia kuumuua mpenzi wake Harieth Robson, aliyedumu naye kwa muda kabla ya balaa hilo.
.
Nyota huyo aliachiwa huru kwa dhamana baada ya kukamatwa, huku kesi yake ikipangwa kusikilizwa Juni 23, mwaka huu na mahakama ya Salford Magistrates, iliyopo jijini Manchester.
 
MMEMSIKIA PEREZ KUHUSU HAALAND
.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, amesisitza Erling Haaland, angeanzia benchi kutokana na ubora wa Karim Benzema, endapo angejiunga na mabingwa hao wa Ulaya msimu uliyopita.
.
“Hatukupata shida tulipomkosa Kylian Mbappe na Haaland, tuna Benzema na ilikuwa ngumu Haaland kusajiliwa, huwezi kumsajili mchezaji halafu akae benchi, ni mchezaji mzuri na anastahili kucheza kila mechi,” alisema Perez.
 
KAIFIKIA BUANA !!
.
Kwa kufunga mabao mawili dhidi ya Coastal Union juzi, straika wa Yanga, Fiston Mayele [emoji1078] ameifikia rekodi ya mfungaji bora wa ligi msimu uliopita, John Bocco [emoji1241] wa Simba aliyefunga mabao 16.
.
Je, atafanikiwa kuivunja __!![emoji102]
 
[emoji599]BREAKING: SIMBA YAMUUZA BWALYA
.
Uongozi wa Simba umethibitisha kuwa umefikia makubaliano ya kumuuza kiungo mshambuliaji Rally Bwalya [emoji1268]. Kwa mujibu wa taarifa Simba itautumia mchezo wa Jumapili dhidi ya KMC utakaofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa kumuaga rasmi nyota huyo raia wa Zambia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…